Bosco Ntaganda.
Aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amekanusha mashtaka yaliyokuwa yakimkabili ya uhalifu wa kivita na ukatili dhidi ya binadam, baada ya kufikishwa katika mahakama ya Kimataifa ya jinai, ICC, iliyoko mjini the Haque.
Bosco Ntaganda anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya zaidi ya raia mia nane na kuwabaka watoto waliokuwa wamesajiliwa jeshini kama watumwa wa ngono.
Mashtaka yote yanahusiana na wakati alipokuwa akiongoza mapigano katika eneo la Ituri Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwaka wa 2002 na 2003.
Ntaganda Ntaganda anatarajiwa kukutana ana kwa ana na baadhi ya watu walioadhirika wakati waa vita hivyo.
Baada ya miaka kadhaa ya mapigano, Ntaganda alijisalimisha mwaka wa 2013, katika ubalozi wa Marekani nchini Rwanda na kutaka kuwasilishwa kwa mahakama ya ICC.
Ntaganda alijulikana na The Terminator na watu wengi humtambua kutokana na jinsi anavyolinda ndevu zake na kofia kubwa kubwa na jinsi anavyopenda maisha ya starehe.
Ntaganda anakabiiwa na mashtaka 18 yakiwemo mauaji, ubakaji na usajili wa watoto jeshini.
Awali Bensouda alimtaja Bosco Ntaganda kama mtu mwenye sifa mbaya.
|
No comments:
Post a Comment