DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Monday, December 28, 2015

RAIS MAGUFULI AKAMILISHA BARAZA LAKE KWA KUWAAPISHA MAWAZIRI WATANO NA NAIBU WAZIRI MMOJA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Desemba 28, 2015 Baraza la Mawaziri la Serikali ya awamu ya tano limekamilika baada ya Mawaziri watano na Naibu Waziri mmoja kula viapo, shughuli imefanyika Ikulu Dar es salaam ikiongozwa na Rais John Pombe Magufuli.
Prof. Jumanne Maghembe-Waziri Maliasili na Utalii.
Prof. Makame Mnyaa Mbarawa-Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Mhandisi Gerson Lwenge-Waziri wa Maji na Umwagiliaji.
Dkt. Philip Mpango-Waziri wa Fedha na Mipango.
Dkt. Joyce Ndalichako-Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
Hamad Masauni-Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

LIONEL MESSI ASHINDA TUZO ZA GLOBE SOCCER AWARDS 2015,


Ikiwa ni siku kadhaa zimepita toka gazeti la Hispania la Marca litangaze orodha ya wachezaji kumi bora kwa mwaka 2015 ikiongozwa na Lionel Messi ikifuatiwana Neymar na Cristiano Ronaldo kutajwa kuwa nafasi ya nane. Desemba 27, 2015 Lionel Messi ametajwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2015 (Globe Soccer Awards) inayotolewa kila mwaka.
Globe Soccer Awards 2015 zilizotolewa Dubai ni tuzo maalum kwa ajili ya wanasoka, viongozi bora wa klabu, wakala bora, kocha bora. Hizi ni tuzo ambazo zinatolewa kwa uandaaji au ushirikiano wa chama cha mawakala wa wachezaji soka barani Ulaya EFAA (European Association of Player’s Agents) na umoja wa vilabu vya soka barani Ulaya ECA (European Club Association). Hii ndio list ya washindi wa tuzo hizo kwa mwaka 2015.

  • Lionel Messi (Mchezaji bora wa mwaka)
  • FC Barcelona (Klabu bora kwa mwaka)
  • Jorges Mendes (Wakala bora wa mwaka)
  • Marc Wilmots (Kocha bora wa mwaka)
  • S.L BENFICA (Acadeny bora ya mwaka)
  • Ravshan Irmatov (Refa bora wa mwaka)
  • Josep Maria Bartomeu (Rais bora wa klabu)
  • Andrea Pirlo (Life time Archivement)
  • Frank Lampard (Life time Archivement)

MWANDISHI NA MPIGA PICHA MAARUFU NCHINI EDWIN MJWAHUZI AAGA UKAPERA




















JAPAN YAKUBALI FIDIA KWA WATUMWA WA NGONO

Waziri wa kigeni wa Japan Fumio Kishida (kushoto) asalimiana na mwenzake wa Korea Kusini Yun Byung-se
Japan na Korea Kusini zimefikia makubaliano ya kihistoria kuhusu wanawake waliolazimishwa kuhudumu katika madanguro kama watumwa wa ngono wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
Japan imeomba msamaha na kukubali kulipa yen 1bn ($8.3m, £5.6m) ambazo zitawekwa kwenye hazina ya waathiriwa itakayosimamiwa na Korea Kusini.
Mzozo huo umeathiri uhusiano kati ya mataifa hayo mawili, Korea Kusini ikitaka kuombwa msamaha “kwa dhati” na kutolewa kwa fidia kwa waathiriwa.
Mwafaka wa sasa ndio wa kwanza kuhusu suala hilo tangu 1965 na umepatikana baada ya pande zote mbili kuahidi kuharakisha mazungumzo.
Tangazo hilo limetolewa baada ya waziri wa mashauri ya kigeni wa Japan Fumio Kishida kuwasili Seoul kwa mashauriano na mwenzake Yun Byung-se.
Baada ya mkutano Kishida aliambia wanahabari kwamba Waziri Mkuu Shinzo Abe ameomba msamaha kutoka kwa “wote walioathirika”.
Wanawake takriban 200,000 walilazimishwa kuwa watumwa wa ngono kwa wanajeshi wa Japan wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, wengi wao wakitoka Korea.
Ni 46 pekee kati yao walio hai Korea Kusini.
Wengine walitoka Uchina, Ufilipino, Indonesia na Taiwan.
Wanaharakati wa kutetea wanawake hao waliweka sanamu ya msichana waliyoiita "Sanamu ya Amani" nje ya ubalozi wa Japan Seoul mwaka 2011
Japan ilikuwa awali imekubali lawama kwenye taarifa iliyotolewa 1993 na katibu wa baraza la mawaziri wa wakati huo Yohei Kono.
Hazina ya kibinafsi ilianzishwa 1995 kwa ajili ya waathiriwa na ikadumu kwa mwongo mmoja.
Pesa hizo hata hivyo zilitoka kwa michango ya wahisani na si kutoka kwa serikali ya Japan. CHANZO: bbcswahili.com

MR. FLAVOUR KUFUNGA NDOA LEO?

Mkali wa nyimbo za AshawGolibna Sweetie Mr Flavour, asubuhi ya Desemba 27, 2015 amekuwa gumzo nchini kwao Nigeria, baada ya kuaminika kuwa staa huyo yupo katika mipango ya kufunga ndoa ya siri siku ya leo Desemba 28, 2015.
Mr. Flavour anatajwa kutaka kumuoa mpenzi wake wa kwanza Sandra Okagbue kwa siri akiwa na lengo la kuepuka mzozo na mpenzi wake wa zamani Anna Banner pamoja na familia yake ambao hawana taarifa za kuwa jamaa amepanga kuoa.
Staa huyo wa wimbo wa Ashaw ambaye alishirikishwa na Diamond Platnumz wa Tanzania katika wimbo wa Nana, hayupo ndani ya Nigeria anatajwa kuwa alisafiri kwa ajili ya kwenda kusherehekea Sikukuu ya Noeli (Chrismass). Mr. Flavour anatajwa kurudi jana Desemba 27, 2015) na kupanda ndege kuelekea Onitisha sehemu ambayo harusi yake ya kimila itafanyika. Uongozi wa Mr. Flavour umekaa kimya juu ya taarifa hizo kwa kutosema chochote licha ya chanzo cha habari hizi kusema kuwa tayari marafiki wa Mr Flavour wana mualiko. CHANZO: millardayo.com

ARSENAL YABAMIZWA 4-0 NA SOUTHAMPTON

Kiungo wa Southampton Steven Davis (kulia) akiwania mpira na kiungo mkabaji wa Arsenal Mathieu Flamini kwenye mtanange huo.
Cuco wa Southampton akishangilia goli la kwanza dhidi ya Arsenal.
Wachezaji wa Arseal wakiwa hawaamini kinachoendelea.


Mshambuliaji wa Southampton Shane Long akipachika kimiani goli la pili.

Theo Walcott(kushoto) akikabiliana na mchezaji wa Southampton.

BURUNDI YASEMA MAZUNGUMZO YA AMANI KUANZA KAMPALA

Mazungumzo ya kusuluhisha mzozo wa Burundi yataanza tena kesho mjini Kampala, chini ya usimamizi wa Rais Yoweri Museveni wa Uganda.
Museveni aliteuliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki kuongoza mchakato wa amani ya Burundi, kufuatia machafuko yaliyozushwa na uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza kupigania muhula wa tatu, kinyume cha maana ya mapatano ya Arusha na katiba ya Burundi inayoruhusu mihula miwili.
Mamia ya Warundi wanasemekana kuuawa na maelfu kukimbia makwao.
Makundi 14, yakiwakilisha masilahi mbalimbali ya Warundi, yatashiriki mkutanoni.
Mwandishi wa BBC wa Kampala, Alli Mutasa, anaripoti kuwa sababu mazungumzo ya amani ya Burundi yamekawia kuanza, hadi Desemba 28, ilitokana na shida ya kuyajumuisha makundi yote husika, kwa mujibu wa Waziri wa Ulinzi wa Uganda, Crispus Kiyonga.
“Haikuwa rahisi,” alisema. Na baada ya kuzinduliwa rasmi mjini Kampala leo, mazungumzo hayo yatahamishiwa Arusha Tanzania, ila pakizuka neno.
Chama tawala CNDD-FDD na makundi kadha dhidi ya serikali ya Nkurunziza, vitahudhuria aliongeza Dk Kiyonga.
Mamia ya Warundi wanasemekana kuuawa na maelfu kukimbia makwao.
Agenda ya mazungumzo haijulikani wazi.
Bila shaka amani ndio kiini cha mazungumzo haya, na vipi ipatikane.
Zaidi ya wiki moja iliopita, Muungano wa Afrika, ulipendekeza kutuma kikosi cha askari 5,000 ili kukomesha machafuko, na kuzuia Burundi isirudie vita vya wenyewe-kwa-wenyewe na hata wengine kugusia ‘maangamizi ya kimbari’.
Burundi inalaani mashauri hayo kama ‘uvumi’ uso ‘msingi’, na kukana machafuko yamefika hadi hio.
Serikali inashikilia kuna amani nchini ila sehemu fulani-fulani za mji mkuu Bujumbura.
Hivyo serikali si tayari kukikubali kikosi cha Muungano wa Afrika, na kikipelekwa kwa kifua, kitakabiliwa kama cha ‘uvamizi’.
Tanzania, ambayo ina maelfu ya wakimbizi Warundi, pia inapinga kikosi cha Muugano wa Afrika kutumwa Burundi.
Jumane iliyopita, Waziri mpya wa Nchi za Nje wa Tanzania, Augustine Mahiga, aliunga mkono mazumngumo, sio majeshi ya kigeni, kumaliza machafuko ya Burundi.
Pia aliandama ushauriano wa kidiplomasi kuonana na makundi ya upinzani pamoja na Nkurunziza, Bujumbura, na Museveni Kampala, kwa lengo la kuyafufua mazungumzo hayo ya amani.
Umoja wa Ulaya umechangia dola laki nne unusu kuwezesha mazungumzo ya Burundi yarudiwe.
Zaidi ya watu 400 wanaripotiwa kufa katika machafuko yalioanza Aprili mwaka huu, na kama Warundi laki tatu, ni wakimbizi wa nje na ndani ya nchi. CHANZO: BBC

Friday, December 25, 2015

JURGEN KLOPP ALALAMIKIA RATIBA YA LIGI KUU ENGLAND

Meneja wa Timu ya Liverpool Jurgen Klopp amelalamikia mfululizo wa mechi wakati wa Krismasi hadi kuingia Mwaka Mpya ya Ligi Kuu England kunaiumiza England kufanya vizuri katika mashindano makubwa.
Mjerumani huyo amekiri kuwa Wachezaji wa England wana vipaji vikubwa lakini kwa kukosa Vakesheni hii ya wakati huu wa Majira ya Baridi kutaiathiri England Mwezi Juni kwenye Fainali za Mataifa ya Ulaya, EURO 2016, zitakazochezwa Nchini France.
Akiongea kwenye Kipindi cha Football Focus cha BBC, Klopp amesema, Kwa hakika, mna Gemu nyingi mno, Hamna Mapumziko, mna Mashindano mengi.
Klopp ameeleza, kuwa England chini ya Meneja Roy Hodgson, wanapaswa kutwaa EURO 2016 kwa vile wana vipaji vikubwa.
Klopp pia amesema hali hiyo inaathiri Vilabu vya England kushinda kwenye Mashindano ya Vilabu ya UEFA.
Hivi sasa Ligi zote kubwa Ulaya, La Liga ya Spain, Bundesliga ya Germany na Serie A ya Italy, pamoja na nyingine kadhaa, zipo Vakesheni ya Krismasi na Mwaka Mpya.
Ndani ya siku nane Kikosi cha Liverpool chini ya Klopp kinakabiliwa na Mechi 3 kuanzia Jumamosi watakapokuwa kwao Anfield kuwavaa Vinara wa Ligi Leicester City. CHANZO: BBCSWAHILI.COM

ROONEY AWAASA WACHEZAJI WENZAKE KUNUSURU KIBARUA CHA LOUIS VAN GAAL

Nahodha wa Manchester United Wayne Rooney amewashauri wachezaji wenzake kukaza buti ili kuokoa kibarua cha meneja wao Louis van Gaal.
Kufuatia kutoshinda katika Mechi 6 zilizopita na kutupwa nje ya michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kibarua cha Van Gaal kimekuwa kwenye hatari kubwa.
Klabu hiyo imeporomoka hadi nafasi ya 5 kwenye Ligi Kuu England na kujikuta wakiwa na Pointi 9 nyuma ya vinara Leicester City,
Rooney amenukuliwa akisema: "Hatujashinda katika wiki chache zilizopita na ni kawaida kupoteza kujiamini. Inabidi turejeshe imani kwani tuna michezo migumu na tunahitaji tuwe bora zaidi. Si kitu chema kufungwa kila mchezo. Ni ngumu kwa wachezaji. Tunaumia kwani sisi ni watu wa fahari na tunajionea fahari kuichezea Manchester United." CHANZO: BBCSWAHILI.COM

PAPA FRANCIS AWATAKA WAKRISTO DUNIANI WASIONGOZWE NA MALI, AWATAKA KUWA WANYENYEKEVU

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amewashauri waamini 1.2 bilioni kanisa hilo “wasileweshwe” na mali na utajiri.
Akitoa mahubiri yake ya kila mwaka siku ya Krismasi, Papa Francis amewataka wafanye mambo kwa kiasi. Amesema ulimwengu wa sasa umetawalia na “kutumia mali kwa wingi, anasa na utajiri”.
Papa alikuwa akiongoza maadhimisho ya mkesha wa Krismasi katika kanisa la Mt. Petro mbele ya waamini takriban 10,000.
Baadaye leo Ijumaa, atatoa ujumbe wa kila mwaka wa Krismasi kutoka kwenye roshani ya mida ya kanisa hilo la St Peter's.
Alipokuwa akiongoza ibada ya misa, Papa alisema Krismasi ni wakati mwingine wa kujitambua na kujitafakari.
Aliwahimiza waumini kuonyesha maisha ya ukawaida kama alivyofanya mtoto Yesu, “alipozaliwa katika maisha ya ufukara katika zizi la ng’ombe licha ya utukufu wake” kama mwongozo katika maisha yao.
“Katika jamii hii ambayo kawaida imeleweshwa na mtindo wa kutumia mali kwa wingi, anasa na utajiri, mtoto huyu anatuhimiza tufanye mambo kwa kiasi, kwa njia ambayo ni rahisi, ya kufanya mambo kwa kipimo, na kufanya mambo yaliyo ya muhimu,” alisema.
“Katika utamaduni huu wa siku hizi wa kutojali ambao mara nyingi hugeuka na kuwa ukatili, mtindo wetu wa maisha unafaa kuwa wa kujitolea, upendo, kuhurumia wengine na msamaha.”
Usalama uliimarishwa wakati wa ibada hiyo na polisi walikuwa wakipekua watu na magari maeneo yaliyo karibu na Vatican.
Wote walioingia kwenye kanisa hilo, ambalo ndilo kubwa zaidi duniani, walilamika kupitia kwenye mitambo ya kupekuwa watu kutambua vyuma.
Waandishi wa habari wanasema Papa Francis, 79, alitumia mahubiri hayo kuangazia mada kuu ambazo ameangazia katika uongozi wake – msamaha, huruma, kuhisi hisia za watu wengine na kutenda haki.
Sauti yake ilikuwa hafifu wakati mwingine, kutokana na mafua yaliyokuwa yamempata mapema wiki hii.

Monday, December 21, 2015

ABIRIA 2 WA AIR FRANCE WAKAMATWA PARIS KUFUATIA TISHIO LA BOMU IKIWA ANGANI

Abiria 2 wakamatwa Paris
Maafisa wa polisi nchini Ufaransa wamewatia mbaroni mume na mkewe waliokuwa abiria katika ndege ya Air France iliyolazimika kutua kwa dharura nchini Kenya hapo jana kufuatia tishio la bomu ikiwa angani.
Duru zinasema kuwa wawili hao ambao majina yao bado hayajatangazwa hadharani walikamatwa punde baada ya kutua katika uwanja wa kimataifa wa Charles de Gaulle.
  • Yamkini waliokamatwa ni afisa mmoja mstaafu wa polisi ambaye ni mshukiwa mkuu huku mkewe akitumika kama shahidi.
  • Mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege la Air France alifutilia mbali tahadhari ya' bomu' iliyosababisha ndege ya kutua Kenya kuwa ni bandia.
Ndege hiyo ilikuwa na abiria 459 na wahudumu 14.
Frederic Gagey aliwaambia waandishi wa habari mjini Paris Ufaransa kuwa kifaa kilichodhaniwa kuwa kilipuzi kilikuwa ni mbao na kisanduku cha karatasi tu wala hakikuwa na uwezo wowote wa kuhatarisha usalama wa ndege hiyo.
Ndege hiyo ya Ufaransa chapa Boeing 777 nambari AF463 inayohudumu kati ya Mauritius na Paris ililazimika kutua baada ya kile kinachotajwa kuwa bomu bandia.
Inasemekana kuwa abiria mmoja alikipata kifaa hicho chooni na akamfahamisha mhudumu mmoja wa ndege hiyo.
  • Ndege hiyo ilikuwa na abiria 459 na wahudumu 14.
Mume na mkewe wamekamatwa walipotua mjini Paris
Mhudumu huyo alimfahamisha rubani kuhusiana na kifaa hicho na shughuli za kutua kwa dharura zikaanza.
Ndege hiyo ilitua saa sita usiku wa kuamkia Jumapili, huku wataalamu wa kutegua mabomu kutoka jeshi la wanamaji la Kenya wakiingia ndani ya ndege hiyo kukagua kifurushi kilicholeta taharuki.
Sasa kitengo cha ujasusi cha Ufaransa kimeanzisha uchunguzi wa kina kubaini kilichosababisha tishio hilo. CHANZO: BBC

FIFA YAANIKA BLATTER NA PLATINI NJE KWA MIAKA 8

Maafisa wawili wakuu zaidi katika usimamizi wa kandanda duniani rais Sepp Blatter na mwenyekiti wa shirikisho la soka barani ulaya UEFA Michel Platini, wamepigwa marufuku ya miaka 8 ya kutoshiriki kwa vyovyote maswala ya soka kufuatia uchunguzi wa kimaadili.
Wamepatikana na hatia ya ukiukaji wa maswala mbalimbali kama vile kashfa ya dola milioni mbili malipo yasiyo rasmi ambazo zilikabidhiwa Patini mwaka 2011.
Maafisa hao wawili wanasisitiza kutofanya makosa yoyote.
Marufuku hiyo inaanza kutekelezwa mara moja.
Rais huyo wa Fifa tangu mwaka 1998, Bwana Blatter, mwenye umri wa miaka 79, tayari ametangaza kujiondoa katika kinyanganyiro cha kumtafuta rais mpya wakati wa uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo mwezi Februari mwakani.
Naye nahodha wa zamani wa Ufaransa Platini, mwenye umri wa miaka 60, na ambaye alionekana kama kiongozi wa baadaye wa shirikisho hilo, amekuwa akipigiwa upatu wa kuchukua mahala pa Blatter katika uchaguzi mkuu unaopangiwa kufanyika Februari mwakani.
Bingwa huyo mara tatu wa mchezaji bora wa mwaka wa bara Ulaya na nahodha wa zamani wa Ufaransa, amekuwa Rais wa UEFA tangu mwaka 2007.
Kauli hii ya kamati ya maadili inaonekana kukatiza taaluma yao katika kandanda .
Blatter na Platini pia wamepigwa marufukuya dola elfu arobaini ($40,000) na ($80,000) mtawalia.
Blatter amesema kuwa atakwenda katika mahakama ya maswala ya michezo (Court of Arbitration for Sport) iliyoko Lausanne kukata rufaa.
Blatter anasema kuwa malipo hayo yalikuwa ya kazi aliyomfanyia lakini kamati ya uadilifu na nidhamu ya FIFA imewapata na hatia ya kuwa yalikuwa malipo ya kiinua mgongo.
Kamati ya uadilifu na nidhamu hata hivyo imewapata na hatia ya kutoa pesa na kuingia katika kandarasi kinyume na maadili ya FIFA.