DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Friday, December 04, 2015

NHIF YAZINDUA RASMI KITUO CHA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA WATEJA KWA NJIA YA SIMU ZA KIGANJANI

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Michael Mhando akizungumza na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano na Huduma Kwa Wateja (Call center) ambacho kitahusika na kupokea na kujibu hoja za wadau mbalimbali zitakazowasilishwa katika Mfuko kupitia Namba ya simu 0800 110063, barua pepe info@nhif.or.tz na mawasiliano kwa njia ya mtandao (Mitandao ya kijamii na simu za mkononi), uliofanyika Desemba 03, 2015 kwenye makao makuu ya Mfuko huo, jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Rehani Athumani (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano na Huduma Kwa Wateja (Call center) ya NHIF, uliofanyika Desemba 03, 2015 kwenye makao makuu ya Mfuko huo, jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Michael Mhando akionyesha kipeperushi chenye namba ya mawasiliano ya moja kwa moja na kituo hicho.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Michael Mhando (kulia) na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya SoftNet Tech, Nuru Yakub Othman wakishirikiana kuzindua rasmi Kituo cha Mawasiliano na Huduma Kwa Wateja (Call center) cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, uliofanyika jana kwenye makao makuu ya Mfuko huo, jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Michael Mhando (kushoto) akimuangalia Ofisa Uanachama wa Kituo cha Mawasiliani ya Huduma kwa wateja, Eva Mkwizu wakati akiwasiliana na wateja wa njia ya simu. Katikati ni Mkurugenzi wa Utawala wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Beatus Chijumba.
Baadhi ya Maofisa Uanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakiendelea kutoa huduma katika kituo hicho.


No comments:

Post a Comment