Meneja wa klabu ya Chelsea ya
Uingereza, Jose Mourinho amefutwa kazi baada ya klabu hiyo kuandikisha msururu wa matokeo
mabaya.
Bodi ya klabu hiyo ilikutana
jana kujadili hatima ya Mourinho chini ya mmiliki wa klabu hiyo, Mrusi Roman
Abramovich.
Mreno huyo mwenye umri wa
miaka 52 amekuwa Chelsea kwa kipindi cha pili, kilichoanza Juni 2013.
Chelsea walimaliza alama nane
mbele kileleni msimu uliopita na kutwaa taji pamoja na Kombe la Ligi lakini
mwaka huu wameanza vibaya, wakishindwa mechi tisa kati ya 16 hadi kufikia sasa.
Mechi ya mwisho kwa Mourinho
kwenye usukani ilikuwa Jumatatu walipochapwa na viongozi
wa ligi Leicester City 2-1.
Pep
Guardiola, Guus Hiddink,
Brendan Rodgers na Juande Ramos ni miongoni mwa wanaopigiwa chapuo
kurithi mikoba yake ili wainusuri miamba hiyo na kushuka daraja.
|
No comments:
Post a Comment