Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya England Chelsea kwa sasa haina kocha baada ya kumfukuza kazi kocha wao mkuu Jose Mourihno.
Headlines za sasa zimemgeukia kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Ulolanzi Guus Hiddink ambaye ametajwa kukaimu nafasi ya Mourinho na tayari amesafiri kwa ndege leo kwenda kufanya mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo.
Hiddink, aliwahi kunoa Chelsea na kuwasaidia kushinda Kombe la FA mwaka 2009, lakini bado hawajafikia makubaliano ya mkataba.
Pia Hiddink alishinda mataji sita ya ligi ya Uholanzi na Kombe la Ulaya akiwa meneja wa PSV Eindhoven ya Uholanzi katika vipindi viwili. |
No comments:
Post a Comment