Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amewashauri waamini 1.2 bilioni kanisa hilo “wasileweshwe” na mali na utajiri.
Akitoa
mahubiri yake ya kila mwaka siku ya Krismasi, Papa Francis amewataka
wafanye mambo kwa kiasi. Amesema ulimwengu wa sasa umetawalia na
“kutumia mali kwa wingi, anasa na utajiri”.
Papa alikuwa akiongoza maadhimisho ya mkesha wa Krismasi katika kanisa la Mt. Petro mbele ya waamini takriban 10,000.
Baadaye leo Ijumaa, atatoa ujumbe wa kila mwaka wa Krismasi kutoka kwenye roshani ya mida ya kanisa hilo la St Peter's.
Alipokuwa akiongoza ibada ya misa, Papa alisema Krismasi ni wakati mwingine wa kujitambua na kujitafakari.
Aliwahimiza
waumini kuonyesha maisha ya ukawaida kama alivyofanya mtoto Yesu,
“alipozaliwa katika maisha ya ufukara katika zizi la ng’ombe licha ya
utukufu wake” kama mwongozo katika maisha yao.
“Katika jamii hii
ambayo kawaida imeleweshwa na mtindo wa kutumia mali kwa wingi, anasa na
utajiri, mtoto huyu anatuhimiza tufanye mambo kwa kiasi, kwa njia
ambayo ni rahisi, ya kufanya mambo kwa kipimo, na kufanya mambo yaliyo
ya muhimu,” alisema. |
No comments:
Post a Comment