DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Monday, December 07, 2015

RAIS MAGUFULI AENDELEA KUISUKA BANDARI

Mpaka leo hii Disemba 07, 2015 tunahesabu mwezi mmoja hivi umepita tangu Rais Magufuli aapishwe na aanze kazi ya Urais wa awamu ya tano Tanzania.
Mfululizo wa habari zenye uzito wa kasi yake kwenye Urais zimekuwa zikitufikia kila siku, ya leo bado inabeba uzito mara nyingine… tangu siku ya kwanza Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa amefanya ziara ya ghafla bandarini mengi yameripotiwa ikiwemo suala la ubadhirifu, rushwa, kukwepa kodi ya upotevu wa makontena.
Mpya kutoka bandarini inahusu kutenguliwa kwa uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi wa bandari, Awadhi Massawe, na pia kuvunja bodi ya bandari Dar es Salaam.
Kingine ni kwamba Rais Magufuli pia amemsimamisha kazi Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Shabani Mwanjaka. CHANZO: millardayo.com

No comments:

Post a Comment