DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Friday, December 18, 2015

RC DOM AZINDUA MASHINDANO YA MICHEZO VYUO VIKUU NA ELIMU YA JUU NCHINI

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku  Gallawa akikagua timu za mpira wa miguu za chuo kikuu cha Eckernforde Tanga na State University Zanzibar  wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya michezo ya vyuo vikuu na elimu ya Juu Tanzania yanayoendelea kufanyika mjini Dodoma.
Wanamichezo kutoka vyuo vikuu na elimu ya juu hapa nchini wakiwa kwenye maandamano ya kusherehekea uzinduzi wa mashindano ya michezo ya vyuo vikuu na elimu ya juu yanayoendelea kufanyika Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akipiga mpira wa adhabu (penalty) kuashiria ufunguzi rasmi wa mashindano ya michezo ya vyuo vikuu na elimu ya juu hapa nchini yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya UDOM mjini Dodoma.


No comments:

Post a Comment