Maafisa wawili wakuu zaidi katika
usimamizi wa kandanda duniani rais Sepp Blatter na mwenyekiti wa
shirikisho la soka barani ulaya UEFA Michel Platini, wamepigwa marufuku
ya miaka 8 ya kutoshiriki kwa vyovyote maswala ya soka kufuatia
uchunguzi wa kimaadili.
Wamepatikana na hatia ya ukiukaji wa
maswala mbalimbali kama vile kashfa ya dola milioni mbili malipo yasiyo
rasmi ambazo zilikabidhiwa Patini mwaka 2011.
Maafisa hao wawili wanasisitiza kutofanya makosa yoyote.
Marufuku hiyo inaanza kutekelezwa mara moja.
Rais
huyo wa Fifa tangu mwaka 1998, Bwana Blatter, mwenye umri wa miaka 79,
tayari ametangaza kujiondoa katika kinyanganyiro cha kumtafuta rais mpya
wakati wa uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo mwezi Februari mwakani.
Naye
nahodha wa zamani wa Ufaransa Platini, mwenye umri wa miaka 60, na
ambaye alionekana kama kiongozi wa baadaye wa shirikisho hilo, amekuwa
akipigiwa upatu wa kuchukua mahala pa Blatter katika uchaguzi mkuu
unaopangiwa kufanyika Februari mwakani.
Bingwa huyo mara tatu wa
mchezaji bora wa mwaka wa bara Ulaya na nahodha wa zamani wa Ufaransa,
amekuwa Rais wa UEFA tangu mwaka 2007. |
No comments:
Post a Comment