Rais wa Rwanda Paul Kagame ametetea
uamuzi wa taifa hilo kuandaa kura ya maoni kuhusu muhula wa rais akisema
lilikuwa wazo la Wanyarwanda.
Raia nchini humo wamepiga kura leo kuhusu marekebisho ya katiba ambayo huenda yakamuwezesha Bw Kagame kutawala hadi 2034.Alipoulizwa na mwandishi wa BBC Catherine Byaruhanga kuhusu wazo la kubadilisha katiba, Bw Kagame alijibu: “Sikuomba hili lifanywe, nenda kawaulize Wanyarwanda mbona wakajiingiza katika hili.” Bw Kagame hata hivyo alisema ukiangalia rekodi yake uongozini “labda unaweza kupata wazo na kujua ni yapi yanatarajiwa.” Kiongozi huyo bado hajatangaza iwapo atawania tena baada ya muhula wake kumalizika 2017, na amesisitiza kwamba atatangaza hilo baada ya kura ya maoni. Lakini kuhusu mipango yake ya siku za usoni kuhusu Rwanda amesema: “Wana (Wanyarwanda) mustakabali gani? Si mimi ninayedhibiti mustakabali wao. Wanashikilia hatima yao mikononi.” Bw Kagame alipiga kura katika kituo cha Rugunga mjini Kigali. Wapiga kura walikuwa wakipigia marekebisho ya katiba ya 2015, na miongoni mwa mengine kupunguza muda wa rais kuhudumu kuwa mihula miwili ya miaka mitano badala ya saba. |
Friday, December 18, 2015
KAGAME ASEMA KUFANYIKA KWA KURA ZA MAONI NI WAZO LA WANYARWANDA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment