Diamond akiwa kapozi na mpenzi wake Zari.
Sasa
hivi kwenye ulimwengu wa muziki, gumzo ni ngoma aliyoitoa Mwanamuziki
Nasibu Abdul ‘Diamond’ inayokwenda kwa jina la Utanipenda. Ni ngoma kali
ambayo itatambulishwa kwa mara ya kwanza ndani ya Ukumbi wa Kimataifa
wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar.
Mbali
na utambulisho wa ngoma hii ambayo itapigwa live kwa kutumia vyombo,
nyimbo nyingine ambazo Diamond atazipiga siku hiyo ni pamoja na
Mdogomdogo, Nasema Nawe, Nana na nyinginezo zinazobamba huku akiwa na
madansa wake kutoka Wasafi Classic Baby (WCB). Itakuwa ni siku ya
Krismasi (Ijumaaa ijayo) ambayo msanii huyo ameahidi kufanya mambo
makubwa akisindikizwa na mkali wa nyimbo za Singeli, Msaga Sumu pamoja
na wacheza dansi hatari Afrika Mashariki, Wakali Dancers na wasanii
wengine kibao.
Burudani
yote hiyo ambayo imedhaminiwa na huduma kutoka kampuni ya simu
Tanzania, Airtel Money utaipata kwa kiingilio cha shilingi 15,000 tu
getini na wale watakaohitaji huduma ya VIP watalipia shilingi 30,000.
Katika kuelekea kwenye shoo hiyo, Showbiz ilifanikiwa kunasa baadhi ya
picha za nyuma ya pazia ‘behind the scene’ wakati kichupa cha wimbo huo
kikiandaliwa.
Video
hiyo ni mkono wa yuleyule mkali wa vichupa kutoa Sauzi anayekwenda kwa
jina la God Father. Hajakosea! Amefanya bonge la kazi na hata mashabiki
ni mashahidi kwamba wimbo ni mkali na kideo chenyewe ni ‘kitamu’. Maneno
mengi siyo ishu, kwenye hili picha zinaongea zaidi hivyo pitisha macho
kwenye baadhi ya picha hizo ili upate uhondo! Kwani kuna mtu kaibiwa?
Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL
|
No comments:
Post a Comment