Kansela Angela Merkel akiteta jambo na waziri mkuu David Cameron mjini Brussels.
Pia akizunguma baada ya chakula cha usiku walichoshiriki pamoja viongozi
wakuu wa mataifa ya Umoja wa Ulaya, kansela wa Ujerumani Angela Merkel,
alisema itakuwa vigumu kutimiza matakwa ya Uingereza ya kubadilisha
sheria za Umoja wa Ulaya kuhusu mafao kwa wahamiaji, lakini akaongeza
kuwa upo utashi miongoni mwa mataifa wanachama kufikia makubaliano.
"Nilieleza wazi kabisaa kwamba tuko tayari kulegeza msimamo lakini
tutafanya hivyo kwa msingi wa kulinda kanuni za msingi za Ulaya, ambazo
zinajumlisha kutobaguna na uhuru wa kusafiri," alisema Kansela Merkel.
Matumaini ya muafaka
Katika hotuba yake ndefu zaidi katika kipindi cha zaidi ya miaka mitano
ya kuhudhuria mikutano ya kilele ya Umoja wa Ulaya, waziri mkuu David
Cameron aliwambia viongozi wengine 27 wa mataifa ya umoja huo kwamba
ikiwa wanataka kuibakiza Uingereza katika Umoja wa Ulaya, laazima
washughulikie malalamiko ya wapigakura wake kuhusu kudhibiti uhamiaji.
Baada ya mkutano huo w ausiku, Cameron amesema leo kuwa anaona njia ya
kufikia makubaliano.
"Ninachoweza kusema ni kwamba kuna njia ya kufikiwa makubaliano mwezi
Februari. Itahitaji kazi kubwa lakini nilichohisi usiku wa leo kwenye
chumba cha mkutano ni ishara nyingi za nia njema, watu wanataka
makubaliano yatakayoibakiza Uingereza katika Umoja wa Ulaya kwa
kutupatia fursa hiyo kwenye kura yaetu ya maoni. Lakini mengi yanapaswa
kufanywa kati ya leo na wakati huo."
Viongozi wengine walioshiriki katika siku hiyo ya kwanza wa mkutano huo
wa kilele walisema wanataka kumsaidiaCameron kuhakikisha kuwa taifa hilo
lenye uchumi wa pili kwa ukubwa barani Ulaya na moja ya dola kubwa
zaidi kijeshi lnasalia kwenye umoja huo. Lakini wengi walisisitiza
kwamba suala la mabadiliko katika mikataba ya Umoja wa Ulaya halina
mjadala.
Viongozi hao pia walikubaliana kuharakisha uundwaji wa kikosi cha ulinzi
wa mipaka ya nje ya Umoja wa Ulaya, na kuhimizana kutekeleza hatua
zilizokubaliwa mwaka huu kupunguza uhamiaji wa kuvuka bahari ya
Mediterrani.
Mwandishi: Iddi Ssessanga/rtre,dpae,
Mhariri: Saumu Yusuf
|
No comments:
Post a Comment