DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Friday, December 04, 2015

TANZANIA YAPANDA NAFASI 3 VIWANGO VYA FIFA, UBELIGIJI BADO KINARA!

Ubeligiji imebaki ambari Wani kwenye FIFA orodha ya Ubora Duniani iliyotolewa Leo huku Tanzania ikipanda Nafasi 3. Mabingwa wa Dunia Ujerumani wameshuka Nafasi 2 na sasa wapo Nafasi ya 4 wakati Argentina wakipinda Nafasi 1 na kushika Nafasi ya Pili na Hispania kupanda Nafasi 3 na kukamata Nafasi ya 3.
Brazili nao wapo Nafasi ya 6 baada kupanda Nafasi 2.
Tanzania sasa ipo Nafasi ya 132 baada ya kupanda Nafasi 3 toka Mwezi uliopita.
Kwa Afrika, Timu ya juu kabisa kwenye orodha ya Ubora ni Ivory Coast ambayo ipo Nafasi ya 19 baada ya kupanda Nafasi ikifuatiwa na Algeria ambayo ipo Nafasi ya 28 baada ya kuporomoka Nafasi 2.
10 BORA:
1. Ubeligiji
2. Argentina [Imepanda Nafasi 1]
3. Hispania [Imepanda Nafasi 3]
4. Ujerumani [Imeshuka Nafasi 2]
5. Chile
6. Brazili [Imepanda Nafasi 2]
7. Ureno [Imeshuka Nafasi 3]
8. Colombia [Imeshuka Nafasi 1]
9. Uingereza
10. Austria

No comments:

Post a Comment