DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Friday, December 25, 2015

JURGEN KLOPP ALALAMIKIA RATIBA YA LIGI KUU ENGLAND

Meneja wa Timu ya Liverpool Jurgen Klopp amelalamikia mfululizo wa mechi wakati wa Krismasi hadi kuingia Mwaka Mpya ya Ligi Kuu England kunaiumiza England kufanya vizuri katika mashindano makubwa.
Mjerumani huyo amekiri kuwa Wachezaji wa England wana vipaji vikubwa lakini kwa kukosa Vakesheni hii ya wakati huu wa Majira ya Baridi kutaiathiri England Mwezi Juni kwenye Fainali za Mataifa ya Ulaya, EURO 2016, zitakazochezwa Nchini France.
Akiongea kwenye Kipindi cha Football Focus cha BBC, Klopp amesema, Kwa hakika, mna Gemu nyingi mno, Hamna Mapumziko, mna Mashindano mengi.
Klopp ameeleza, kuwa England chini ya Meneja Roy Hodgson, wanapaswa kutwaa EURO 2016 kwa vile wana vipaji vikubwa.
Klopp pia amesema hali hiyo inaathiri Vilabu vya England kushinda kwenye Mashindano ya Vilabu ya UEFA.
Hivi sasa Ligi zote kubwa Ulaya, La Liga ya Spain, Bundesliga ya Germany na Serie A ya Italy, pamoja na nyingine kadhaa, zipo Vakesheni ya Krismasi na Mwaka Mpya.
Ndani ya siku nane Kikosi cha Liverpool chini ya Klopp kinakabiliwa na Mechi 3 kuanzia Jumamosi watakapokuwa kwao Anfield kuwavaa Vinara wa Ligi Leicester City. CHANZO: BBCSWAHILI.COM

No comments:

Post a Comment