Nahodha wa Manchester United Wayne
Rooney amewashauri wachezaji wenzake kukaza buti ili kuokoa kibarua cha
meneja wao Louis van Gaal.
Kufuatia kutoshinda katika Mechi 6
zilizopita na kutupwa nje ya michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya
kibarua cha Van Gaal kimekuwa kwenye hatari kubwa.
Klabu hiyo imeporomoka hadi nafasi ya 5 kwenye Ligi Kuu England na kujikuta wakiwa na Pointi 9 nyuma ya vinara Leicester City,
Rooney
amenukuliwa akisema: "Hatujashinda katika wiki chache zilizopita na ni
kawaida kupoteza kujiamini. Inabidi turejeshe imani kwani tuna michezo
migumu na tunahitaji tuwe bora zaidi. Si kitu chema kufungwa kila
mchezo. Ni ngumu kwa wachezaji. Tunaumia kwani sisi ni watu wa fahari na
tunajionea fahari kuichezea Manchester United." CHANZO: BBCSWAHILI.COM |
No comments:
Post a Comment