DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Friday, December 18, 2015

KIGWANGALLA AWAFUNGIA WAFANYAKAZI NJE YA GETI

Ijumaa ya Desemba 18, 2015 inakuwa siku ya sita tangu Mawaziri na Manaibu wao walioteuliwa na Rais Magufuli na kuapishwa Ikulu Dar es Salaam. Katika baraza hilo, yuko pia Naibu Waziri wa Afya, Dk. Hamisi Andrea Kigwangalla, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nzega Tabora.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram @hamisi_kigwangalla, ameweka picha zinazoambatana na ujumbe unaosomeka ‘Tumefunga geti la ofisi za Wizara ilipofika saa 1:30 asubuhi. Tunataka watumishi wa Wizara wawahudumie wateja wetu Kwa tija na ufanisi'
Sentensi nyingine za Naibu Waziri zinasomeka hivi ‘Mimi nitawajibika kazini. Kila mtu atapaswa kuwajibika. Haya ndiyo mahitaji ya wakati huu. Leo nimefungia wachelewaji kazini nje ya geti. Nitaendelea kushughulika na watoro na watorokaji. Nasubiri ripoti ya watendaji kuhusu trendi ya watumishi wote watoro, wachelewaji kisha nichukue hatua stahiki! Ili kazi ziende ni lazima tuweke nidhamu ya kazi na uwajibikaji maofisini.’ @hamisi_kigwangalla




No comments:

Post a Comment