Mamia ya Warundi wanasemekana kuuawa na maelfu kukimbia makwao.
Agenda ya mazungumzo haijulikani wazi.
Bila shaka amani ndio kiini cha mazungumzo haya, na vipi ipatikane.
Zaidi ya wiki moja iliopita, Muungano wa Afrika, ulipendekeza kutuma kikosi cha askari 5,000 ili kukomesha machafuko, na kuzuia Burundi isirudie vita vya wenyewe-kwa-wenyewe na hata wengine kugusia ‘maangamizi ya kimbari’.
Burundi inalaani mashauri hayo kama ‘uvumi’ uso ‘msingi’, na kukana machafuko yamefika hadi hio.
Serikali inashikilia kuna amani nchini ila sehemu fulani-fulani za mji mkuu Bujumbura.
Hivyo serikali si tayari kukikubali kikosi cha Muungano wa Afrika, na kikipelekwa kwa kifua, kitakabiliwa kama cha ‘uvamizi’.
Tanzania, ambayo ina maelfu ya wakimbizi Warundi, pia inapinga kikosi cha Muugano wa Afrika kutumwa Burundi.
Jumane iliyopita, Waziri mpya wa Nchi za Nje wa Tanzania, Augustine Mahiga, aliunga mkono mazumngumo, sio majeshi ya kigeni, kumaliza machafuko ya Burundi.
Pia aliandama ushauriano wa kidiplomasi kuonana na makundi ya upinzani pamoja na Nkurunziza, Bujumbura, na Museveni Kampala, kwa lengo la kuyafufua mazungumzo hayo ya amani.
Umoja wa Ulaya umechangia dola laki nne unusu kuwezesha mazungumzo ya Burundi yarudiwe.
Zaidi ya watu 400 wanaripotiwa kufa katika machafuko yalioanza Aprili mwaka huu, na kama Warundi laki tatu, ni wakimbizi wa nje na ndani ya nchi. CHANZO: BBC
|