DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Friday, February 20, 2015

WAZIRI CHIKAWE AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA KUPAMBANA NA VURUGU NA UGAIDI

Rais wa Marekani, Barack Obama akitoa hotuba yake katika Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani uliofanyika katika Ukumbi wa Loy Henderson, Wizara ya Mambo ya Nje, jijini Washington DC nchini humo leo. Mkutano huo uliowashirikisha Mawaziri wanaoshughulika na masuala ya usalama kutoka mataifa mbalimbali duniani, Maafisa Waandamizi wa Umoja wa Mataifa (UN), Vyama vya Kiraia na Sekta Binafsi ulijadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupambana na ugaidi pamoja na vurugu mbalimbali dunaini. Katika hotuba yake, Obama alisema mapambano dhidi ya watu wenye msimamo mkali hayawezi kulinganishwa na mapambano dhidi ya waislamu. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe aliiwakilisha Tanzania katika mkutano huo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akimsikiliza kwa makini Rais Barack Obama (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba yake katika Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani uliofanyika katika Ukumbi wa Loy Henderson wa Wizara ya Mambo ya Nje, jijini Washington DC nchini humo leo. Mkutano huo uliowashirikisha Mawaziri wanaoshughulika na masuala ya usalama kutoka mataifa mbalimbali duniani, Maafisa Waandamizi wa Umoja wa Mataifa (UN), Vyama vya Kiraia na Sekta Binafsi ulijadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupambana na vurugu na ugaidi dunaini. Katika hotuba yake, Obama alisema mapambano dhidi ya watu wenye msimamo mkali hayawezi kulinganishwa na mapambano dhidi ya waislamu, hivyo hakuna dini yoyote inayowajibika kwa ugaidi, isipokuwa watu ndio wanaowajibika kwa vurugu na ugaidi. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Rais wa Marekani, Barack Obama akitoa hotuba yake katika Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani uliofanyika katika Ukumbi wa Loy Henderson, Wizara ya Mambo ya Nje, jijini Washington DC nchini humo leo. Mkutano huo uliowashirikisha Mawaziri wanaoshughulika na masuala ya usalama kutoka mataifa mbalimbali duniani, Maafisa Waandamizi wa Umoja wa Mataifa (UN), Vyama vya Kiraia na Sekta Binafsi ulijadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupambana na ugaidi pamoja na vurugu mbalimbali dunaini. Katika hotuba yake, Obama alisema mapambano dhidi ya watu wenye msimamo mkali hayawezi kulinganishwa na mapambano dhidi ya waislamu. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe aliiwakilisha Tanzania katika mkutano huo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kushoto-mstari wa pili), Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula (nyuma ya waziri) wakimsikiliza kwa makini Rais Barack Obama (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba yake katika Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani uliofanyika katika Ukumbi wa Loy Henderson wa Wizara ya Mambo ya Nje, jijini Washington DC nchini humo leo. Mkutano huo uliowashirikisha Mawaziri wanaoshughulika na masuala ya usalama kutoka mataifa mbalimbali duniani, Maafisa Waandamizi wa Umoja wa Mataifa (UN), Vyama vya Kiraia na Sekta Binafsi ulijadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupambana na vurugu na ugaidi dunaini. Katika hotuba yake, Obama alisema mapambano dhidi ya watu wenye msimamo mkali hayawezi kulinganishwa na mapambano dhidi ya waislamu, hivyo hakuna dini yoyote inayowajibika kwa ugaidi, isipokuwa watu ndio wanaowajibika kwa vurugu na ugaidi. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MEZ B AFARIKI DUNIA LEO AKIWA DODOMA

Mez B enzi za uhai wake.                                                                                                                                                         Moja ya taarifa ya kushtua na kuhuzunisha zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii, pamoja na watu kutumiana message ni kuhusu msiba wa aliyekuwa staa wa muziki wa Bongo Fleva, Mez B. Katika kipindi cha LEO TENA cha Clouds FM wametafutwa watu wa karibu ili kuthibitisha taarifa hiyo.
Dada wa marehemu ambaye jina lake ni Rachel amethibitisha kuwa msanii MEZ B amefariki akiwa nyumbani kwao Dodoma.
Noorah ni msanii ambaye walikuwa karibu na Mez B, amesema Mez B alikuwa na homa tangu mwezi December mwaka jana na baadaye akasafiri kwenda Dodoma huku hali yake ikiwa bado sio nzuri, mara ya mwisho wameongea kwenye simu ni siku tano zilizopita, leo simu yake imepokelewa na dada yake akimtaarfu kuwa Mez B amefariki muda mfupi uliopita baada ya kuzidiwa.
Mez B aliwahi kuwa kundi moja Chamber Squad na akina Noorah, Dark Master na marehemu Albert Mangwea pia.
Msiba uko nyumbani kwao eneo la Kisasa, Dodoma. CHANZO: millardayo.com


JOSEPH KUSAGA AFUNGUKA KWENYE POWER BREAKFAST YA CLOUDS FM AKIWA DUBAI

Kwenye Power Breakfast FEB 2015, Mkurugenzi wa Clouds FM amesikika live kutoka Dubai, yako mengi kayazungumza, FIESTA2015, wasanii wa TZ, ishu ya dawa za kulevya, UCHAGUZI 2015 na stori ya Clouds kuuzwa.

Kwanza kuhusu mipango ya Clouds kusikika nchi nzima; “Kwanza nimshukuru sana mwenyezi MUNGU. Kwa yale yote ambayo tuliyaomba na kuwekeza jitihada zetu yametimia, tulikuwa tumebakiza Nachingwea, Kasulu, Simiyu, Geita, Katavi na Njombe… Hiyo Mikoa tumeimilisha that means tumekamilisha kuipiga TANZANIA nzima kama tulivyoahidi mwaka jana
“Sasa hivi tumejaribu kwa kiasi kikubwa sana kuona tunakwenda kwenye upande wa digital zaidi, kuingia kwenye mitandao.. tuna-launch Tanzania Box, Tanzania na dunia nzima watapata nafasi hiyo ya kuweza kuona the biggest OTT in Tanzania. Mtanzania yoyote leo ukiwa na nafasi ukiingia kwenye www.tanzaniabox.com utaona content yote ambayo iko humo ndani“
Fiesta 2015 ipo?;FIESTA ni sherehe kubwa ya burudani.. Fiesta mwaka huu IPO.. iko palepale na tumeipanua zaidi kujaribu kunyanyua utamaduni wa KITANZANIA, vyakula vya kitanzania pamoja na kuipeleka kimataifa zaidi. Ilikuwa tuanze mwaka huu kutoka kwenda kwenye nchi nyingine lakini nafikiria tutaanza kutoka mwaka kesho.. FIESTA iko palepale na nafikiria itakuwa ni bora kuliko miaka yote FIESTA ya mwaka huu..
Kingine ni kuhusu kufanya show nyingine kubwa ya kumleta msanii mkubwa mbali na Fiesta;Tuko katika mazungumzo mazuri kidogo na wasanii wawili watatu ni mapema kuyazungumza, nafikiria kutakuwa na tamasha lingine zaidi ya ambalo litainvolve wasanii wakubwa.. Kuna tamasha lingine litakuja mapema sana pamoja na tamasha la utamaduni
Dubai ni sehemu ambayo ina connection kubwa, hapa anazungumzia ishu ya kuwapeleka wasanii wa Watanzania; “Tuko katika mazungumzo na Diamond pamoja na wasanii wawili wadogo, tunachotaka kufanya ni kuhakikisha wasanii wa Tanzania wakubwa wanawabeba vilevile wasanii wadogo.. Diamond ni shahidi tuko katika mazungumzo ya mwisho ili aweze kuja na wasanii wengine either wa kati au wadogo ili waweze kuwapandisha na wale wadogo wapande..
Kuhusu Uchaguzi Mkuu 2015; “Ni watanzania sisi wenyewe ndio wenyewe jukumu kubwa sana kwanza kujiandikisha kupiga kura and then kuhakikisha kwamba kila Mtanzania anamchagua mtu ambaye kiukweli atampeleka kutoka kwenye level moja kwenda nyingine..“
Hapa anaongelea Clouds kuhusishwa na Chama chama cha CCM; Nimeona kwenye mitandao, yamezungumzwa mengi kuhusu Clouds kuwa radio ya chama tawala CCM.. Mimi mwenyewe sina chama, niko neutral.. Kama kuna individual mmoja au wawili ambao ni mashabiki sio policy ya kampuni.. haturuhusu sisi. Freeman Mbowe ni rafiki yangu wa damu tunafahamiana miaka mingi zaidi ya miaka 30 kwa nini nisimpe nafasi yeye kama naendekeza chama
Kumekuwa na ishu ya mauaji ya albino, hapa anaongelea hilo;Nimeona juzi mtoto mdogo wametoa mikono, miguu nchi inakwenda wapi sasa? Watu wanafikiria maendeleo ni kuuana tena kwa vitu ambavyo havipo. Lazima nchi nzima sasa hivi tuseme kwamba hiyo kitu tunaipiga vita vibaya sana na nafikiria Hashtag inayosema #MimiNitakulinda ingeanza kutumika kwa Watanzania wote sasa hivi na kuhakikisha tunapigana vita kuokoa viumbe ambavyo kiukweli havina hatia
Kesi ya dawa za kulevya na wasanii na vijana TZ; Madawa ya kulevya ni kitu hatari sana.. imewaona watu wengi ambao nimewajua kwa muda mrefu wakiteketea.. Ukiingia umeingia kwenye shimo ambalo hutaweza kuokolewa.. hii vita inatakiwa ipiganiwe na kila mtu. Hawa watu wanaoharibu watoto wetu kwanini wasifuatiliwe? Tunakwenda kuchagua viongozi, lazima tuwe sober na tuwe clean kuanzia sasa mpaka tunapokwenda kuchagua.. #Tanzania2015NoDrugs. Wasanii wangeweza kuwa pamoja na kampeni hizi ingeweza sana kusaidia nchi yetu
Zimeenea stori mitandaoni kuhusu Clouds kuuzwa, hapa anajibu kuhusu hilo;Clouds imejengwa kwa jasho la kuanzia chini.. Hao wakurugenzi watataka kuuza leo baada ya kuhangaika miaka yote 15? It’s impossible, hizo habari hazina ukweli wowote. Sio kampuni moja au mbili au tatu zimetaka kuinunua Clouds, lakini hatujawa tayari tumejitosheleza na tunaweza kuendelea wenyewe bado" CHANZO: millardayo.com

MARAIS WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUKUTANA NAIROBI, KENYA

Bendera ya Jumuia ya Afrika Mashariki

Marais wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanakutana leo mjini Nairobi, Kenya baada ya kutofanyika mkutano wa awali uliokuwa umepangwa kufanyika mwezi Disemba, 2014 mwaka jana mjini Nairobi.
Marais wote watano wa nchi wanachama wanatarajiwa kuhudhuria.
Katika mkutano huo Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania anatarajiwa kukabidhiwa Uenyekiti wa Jumuia hiyo kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, wadhifa ambao alikuwa akabidhiwe mwezi Disemba, 2014, lakini hakuweza kuhudhuria mkutano huo kutokana na kwenda kutibiwa nchini Marekani.
Marais wengine wa nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki ni Yoweri Museveni wa Uganda, Paul Kagame wa Rwanda, Pierre Nkurunzinza wa Burundi, na mwenyeji wa mkutano Uhuru Kenyatta wa Kenya.
Mbali na masuala ya uhusiano wa kiuchumi, kisiasa na kijamii miongoni mwa mataifa hayo, kujadiliwa katika kikao hicho, pia maombi ya nchi za Sudan Kusini na Somalia kuwa uanachama wa jumuia ya Afrika Mashariki yatajadiliwa. CHANZO: BBC

PINDA: TUTAUNGANISHA NGUVU KWA MGOMBEA URAIS ATAKAYETEULIWA NA CCM

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwahutubia wananchi wa Tarafa ya Pawaga.
Waziri Mkuu Pinda akiwapungia mikono wananchi wa Tarafa ya Pawaga.
Wananchi wa Tarafa ya Pawaga wakimshangilia Waziri Mkuu Pinda.

Wananchi wa Tarafa ya Pawaga, Iringa wakimsikiiza Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amewataka watanzania hasa wana Chama wa cha Mapinduzi ( CCM) kuwa na subira katika kumpata mwanachama atakayefaa kusimama kugombea urais kupitia CCM mwaka huu.

Kuwa tayari wengi sana wamejitangaza wazi wazi na wengine wamejitangaza kimya kimya kutaka kugombea Urais na kuwa yote heri ila chama kina utaratibu wake.

" Itafika wakati ambao kila chama kitasema huyu ndie mtu wetu ambae atapambana na vyama vingine...tunachosema sisi huyo atakayependekezwa ndie atakuwa mgombea wetu" alisema Waziri Pinda.

Waziri Pinda alitoa kauli hiyo leo wakati akiwahutubia wakazi wa Tarafa ya Pawaga baada ya kuzindua skimu ya umwagiliji itakayowanufaisha wakazi wa vijiji vitatu kikiwemo cha Magozi, Ilolompya na Mkombilenga uliogharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.6 fedha kutoka kwa wahisani na serikali.

Alisema kuwa utaratibu wa ndani ya chama anbacho wao ni watawala na wanaoendelea kuyafanya maendeleo yanaonekana watalazimika kumuunga mkono atakayeteuliwa na wale wote ambao hawajateuliwa watamuunga mkono atakayeteuliwa kwa makundi yote kuvunjwa na kuwa na Kundi moja pekee.

Kuwa baada ya mgombea wa chama tawala kupatikana jukumu kubwa ni kuwaomba wapenzi wao wote kumchagua huyo aliyeteuliwa na chama.

Hivyo, Pinda aliwataka wananchi kote nchini kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Alisema kuwa zoezi hilo ambalo litawahusu wale wote wenye miaka kuanzia 18 na kuendelea linatarajia kuanza mwezi huu katika Mkoa wa Njombe na kuwa kila kata zoezi hilo litadumu kwa muda wa wiki mbili ama tatu .

"Nawaombeni kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na pia kuipigia kura katiba inayopendekezwa muda ukifika sisi tunaamini ni katiba bora ambayo imegusa makundi yote yakiwemo ya wafugaji na wakulima pamoja na makundi mengine"

Kuwa wapo wapotoshaji ambao watafika na kuwadanganya juu ya katiba hiyo inayopendekezwa na wasiwasikilize.

Alisema kazi kubwa imefanyika katika kuandaa katiba hiyo inayopendekezwa mbali ya wao (UKAWA) kutoka nje wakati wa bunge hilo la katiba lakini wajumbe waliobaki walifanya kazi nzuri ya kuandaa katiba hiyo inayopendekezwa hivyo kuwaomba wananchi kuipigia kura.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Pinda amewataka wakulima wa Mpunga Pawaga katika kuepuka na migogoro kati yao na wafugaji kuweka utaratibu wa kukusanya majani ya Mpunga na kuyapeleka majumbani kwao ili wafugaji wapate kununua kuliko kuyaacha mashambani na kuwafanya wafugaji kuingiza mifugo yao mashambani.


YANGA YAIZABUA PRISONS 3-0 KWA SILAHA ZILE ZILE


Timu ya Yanga jana imepaa kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuibanjua Prison ya Mbeya katika uwanja wake wa nyumbani wa Sokine kwa mabao 3-0.

Mabao ya yanga yalifungwa na wajuzi wale wale walioibanjua katika mchezo wa awali jijini Dar es Salaam  iliposhinda mabao 2-1.



Magoli ya Yanga yamefungwa katika kipindi cha kwanza na  Simon Msuva aliyepachika wavuni goli la kwanza na la tatu huku Andrey Coutinho akifunga goli la pili. 

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1, ambapo bao la kwanza la Yanga lilifungwa na Andrey Coutinho  dakika ya 38, bao la pili lilifungwa na Simon Msuva katika dakika ya 69, huku bao la Prisons likifungwa na Ibrahim Kahaka, katika dakika ya 67.

Ushindi huo umeifanya Yanga kufikisha pointi 48 dhidi ya Azam FC yenye pointi 46 ambayo imelazimishwa sare 0-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.

OMMY DIMPOZ: SIPO KWENYE MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA WEMA

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Omary Nyembo 'Ommy Dimpoz', amesema anashangazwa na uvumi unaoendelea kuwa yupo katika uhusiano na mwigizaji wa filamu, Wema Sepetu.
Akielezea kuhusu picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Ommy Dimpoz, alisema walikuwa Afrika Kusini kwa mapumziko ndipo picha hizo zilipopigwa.
"Tunapiga picha nyingi sana na Wema, hii siyo mara ya kwanza, lakini sijui kwanini hizi zimetengeneza taswira nyingine kwa mashabiki," alisema.
Picha za wawili hao wakiwa katika pozi tofauti zimeendelea kuwa gumzo na kuzua maswali mengi kwa mashabiki, kutokana na ukaribu alionao Ommy Dimpoz na aliyekuwa mpenzi wa zamani wa
Nasib abdul 'Diamond', Wema Sepetu. CHANZO: MTANZANIA

MAMA SALMA KIKWETE ATILIANA SAINI MKATABA WA UPANUZI WA SHULE YA WAMA-NAKAYAMA NA BALOZI WA JAPAN HAPA NCHINI MHE. MASAKI OKADA

Balozi wa Japan nchini Tanzania Mheshimiwa Masaki Okada akizumgumza na Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete pamoja na uongozi wa Taasisi hiyo muda mfupi kabla ya kutiliana saini mkataba wa mradi wa kupanua Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama iliyoko Rufiji, Mkoani Pwani tarehe 19.2.2015.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akitiliana saini na Balozi wa Japan hapa nchini Mheshimiwa Masaki Okada kwenye mradi wa upanuzi wa Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama utakaogharimu dola za kimarekani 498,738. Sherehe ya utiaji saini ilifanyika kwenye ofisi za WAMA zilizopo karibu na Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akibadilishana hati za Mkataba na Balozi wa Japan hapa nchini Mheshimiwa Masaki Okada mara baada ya kutia saini zao kwenye mkataba huo.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akizungumza mara baada ya kumaliza kutiliana saini mkataba wa mradi wa upanuzi wa Shule ya WAMA Nakayama.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Japan hapa nchini Mheshimiwa Masaki Okada mara baada ya viongozi hao kutia saini mkataba wa upanuzi wa Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama. Picha zote na John Lukuwi.

BABA MTAKATIFU FRANSISKO ATOA UJUMBE WA KWARESIMA, 2015

Mtawa wa Kanisa Katoliki Parokia ya Chang'ombe jijini Dar es Salaam, Dafrosa Clement akiwapaka majivu waamini wa Kikristo wa kanisa hilo juzi ikiwa ni ishara ya kuanza safari ya kiroho ya mfungo na majuto kwa ajili ya maandalizi ya Pasaka lakini zaidi sana kwa ajili ya maandalizi ya maisha ya utakatifu milele. 

 ***********

Baba Mtakatifu Fransisko katika ujumbe wake wa Kwaresima kwa mwaka huu, anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema kukabiliana kikamilifu na changamoto zinazojitokeza katika ulimwengu wa utandawazi usiojali wala kuguswa na mahangaiko ya watu. 

 
Baba Mtakatifu anawataka waamini kujifunga kibwebwe ili kupambana dhidi ya tabia ya uchoyo na ubinafsi, inayoendelea kujitanua kiasi hata cha kupata mwelekeo wa kimataifa, kwa kuwabeza watu wanaoteseka, uwepo wa ukosefu wa misingi ya haki na amani. 


Ni tabia inayotaka kumwondoa Mwenyezi Mungu katika maisha ya watu na kusahau kwamba, Mungu ameupenda ulimwengu kiasi hata cha kumtoa Mwanaye wa pekee kwa ajili ya kumkomboa mwanadamu kutoka katika lindi la dhambi na mauti.

Baba Mtakatifu Fransisko anasema kwamba, ni dhamana na jukumu la Kanisa kuhakikisha kwamba, linaacha malango wazi ya mawasiliano kati ya Mwenyezi Mungu na binadamu, kwa njia ya mchakato wa utangazaji wa Habari Njema ya Wokovu, Maadhimisho ya Sakramenti za Kanisa, Ushuhuda wa imani tendaji inayomwilishwa katika matendo ya huruma. Hata pale ulimwengu unapotaka kujifungia na hatimaye kufunga lile lango na mawasiliano kati ya Mungu na ulimwengu, Mwenyezi Mungu bado anaendelea kuonesha jitihada za kumtafuta mwanadamu ili aweze kumwonjesha huruma na upendo wake usiokuwa na kifani.


Kwaresima anasema Baba Mtakatifu, ni kipindi cha mabadiliko, toba na wongofu wa ndani, unaowawezesha Watu wa Mungu kushinda kishawishi cha utandawazi usiojali wala kuguswa na mahangaiko ya watu na badala yake, kujenga utandawazi wa upendo, udugu na mshikamano wa dhati.


Baba Mtakatifu anafafanua mambo mambo makuu matatu yanayopaswa kufanyiwa kazi na Watu wa Mungu ili kuhakikisha kwamba, wanataabikiana na kusumbukiana katika shida na mahangaiko yao, kwani kama kiungo kimoja kinateseka, basi viungo vingine vyote vinateseka pamoja nacho. Huu ni wajibu ambao kwanza kabisa unapaswa kutekelezwa na Kanisa la kiulimwengu, kwa kuonesha umoja wa watakatifu na katika mambo matakatifu. 

Upendo wa Mungu ni silaha madhubuti dhidi ya utandawazi usiojali wala kuguswa na mahangaiko ya watu, ushuhuda wa upendo unaoneshwa na Mama Kanisa kwanza kabisa katika maadhimisho ya Fumbo la Ekaristi Takatifu. Hapa waamini wanakirimiwa neema na baraka ya kuwa ni Ekaristi, yaani Mkate uliomegwa kwa ajili ya jirani zao na hivyo kuwa kweli ni sehemu ya Fumbo la Mwili wa Kristo, yaani Kanisa, hapa ubinafsi na uchoyo havina nafasi tena!


Hatua ya pili katika hija hii ya kipindi cha Kwaresima ni changamoto inayotolewa na Baba Mtakatifu Fransisko katika dhamana na maisha ya Parokia na Jumuiya zake, kwa kuhakikisha kwamba, Kanisa linalosafiri hapa duniani, linaunganika na lile Kanisa la Mbinguni, kwa kuungana pamoja katika sala, huduma na mafao ya wengi, ili kuonesha utukufu wa Mungu. Waamini pia wanapaswa kutambua dhamana na wito wao wa kimissionari, kwa kuvuka mipaka inayowahusianisha na jamii inayowazunguka, tayari kwenda kuwatangazia maskini na wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii, Habari Njema ya Wokovu.

Ni matumaini ya Baba Mtakatifu Fransisko kwamba, Parokia na Jumuiya za Kiparokia ndipo mahali muafaka ambapo Kanisa linaonesha kwa namna ya pekee kabisa utambulisho wake, kwa kuwa ni visiwa vya huruma na upendo wa Mungu kati ya watu wanaozungukwa na bahari kubwa ya utandawazi usiojali wala kuguswa na mahangaiko ya watu.

Baba Mtakatifu anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema akisema “imarisheni mioyo yenu”. Ni jambo la kutisha kabisa kuona jisni ambavyo mwanadamu hana nguvu ya kupambana na mateso pamoja na mahangaiko ya binadamu yanayoendelea kujitokeza kila siku siku ya maisha; lakini wanaweza kuyashinda yote haya kwa njia ya mshikamano wa sala za wengi. Kutokana na changamoto hii, Baba Mtakatifu anawaalika kuungana na Kanisa zima, kwa ajili ya kumtolea Mwenyezi Mungu sala na maombi kwa musa wa masaa 24, tukio litakalofanyika tarehe 13 na tarehe 14 Machi 2015. 


Licha yak usali, waamini wanahamasishwa kuonesha ushuhuda wa upendo kwa njia ya matendo ya huruma kama kielelezo makini cha ushiriki wao katika kuwashirikisha wengine upendo unaoguswa na mahangaiko ya jirani. Baba Mtakatifu anasema kwamba, haiwezekani kwa mwamini kujiokoa peke yake, kwani hiki ni kishawishi cha shetani. Hapa kunahitajika kama anavyosema Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI mchakato wa majiundo ya moyo unaotambua umaskini wake na hivyo kujisadaka kwa ajili ya wengine.

Baba Mtakatifu Fransisko anahitimisha ujumbe wake wa Kwaresima kwa Mwaka 2015 kwa kumwomba Yesu Kristo ili aweze kuifanya mioyo ya waamini kufanana na Moyo wake Mtakatifu, unaosheheni nguvu na huruma; moyo unaokesha na kuonesha ukarimu, ili usije ukatumbukia katika utandawazi usiojali wala kuguswa na mahangaiko ya watu. Kwa ujumbe huu, Baba Mtakatifu anawatakia waamini na watu wote wenye mapenzi mema Kwaresima yenye mabadiliko na mafanikio makuu katika maisha ya kiroho!

KIGOGO CCM AFARIKI GAFLA MKUTANONI

Mwakilishi wa jimbo la Magomeni, Salmin Awadhi Salmin (pichani) amefariki dunia ghafla jana mchana akiwa mkutanoni katika Ofisi Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui Zanzibar.

Salmin Awadh ambaye pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM  na Mnadhimu wa wajumbe wa CCM Baraza la Wawakilishi Zanzibar amefariki wakati akihudhuria vikao vya chama.

Marehemu Awadh alikimbizwa kwa matibabu katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa uchunguzi zaidi. 
Aidha, taarifa kutoka Ofisi ya Katibu wa Baraza la Wawakilishi, iliyotolewa kwa waandishi wa habari kupitia kwa Mkuu wa Idara ya Utawala, Amour Mohamed Amour imesema mwili wa marehemu utaagwa leo saa 5 asubhi katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi na baadae maziko yatakayo fanyika makunduchi.
Dom Land Blog inatoa pole kwa Wana Magomeni, Familia ya Marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na Wazanzibar wote kufuatia msiba huo mzito.

Thursday, February 19, 2015

JK ATEUA WAKUU WA WILAYA WAPYA 27

RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya kwa kuwateua Wakuu wapya 27, kuwahamisha vituo vya kazi 64 na wengine 42 amewabakisha kwenye vituo vyao vya kazi vya zamani.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa OWM TAMISEMI leo mchana (Jumatano, Februari 18, 2015) Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema mabadiliko hayo yamesababishwa na kuwepo kwa nafasi wazi 27 ambazo zilitokana na wakuu wa wilaya watatu kufariki dunia; kupandishwa cheo wakuu wa wilaya watano, kupangiwa majukumu mengine wakuu wa wilaya saba na kutenguliwa kwa uteuzi wa wakuu wa wilaya 12.
Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema, Rais Kikwete amewabadilisha vituo vya kazi wakuu wa wilaya 64 na kuwabakiza kwenye vituo vyao vya zamani wakuu wa wilaya 42.
Wakuu wa Wilaya wapya 27 walioteuliwa ni Mariam Ramadhani Mtima anayeenda Ruangwa; Dk. Jasmine B. Tiisike anayeenda Mpwapwa; Pololeti Mgema (Nachingwea); Fadhili Nkurlu anayeenda Misenyi; Felix Jackson Lyaniva anayeenda Rorya na Fredrick Wilfred Mwakalebela anayeenda wilayaya Wanging'ombe.
Wengine na vituo vyao kwenye mabano ni Zainab Rajab Mbussi (Rungwe); Francis K. Mwonga (Bahi); Kanali Kimiang'ombe Samwel Nzoka (Kiteto), Husna Rajab Msangi (Handeni), Emmanuel J. Uhaula (Tandahimba); Mboni Mhita (Mufindi); Hashim S. Mgandilwa (Ngorongoro); Mariam M. Juma (Lushoto); Thea Medard Ntara (Kyela); Ahmad H. Nammohe (Mbozi); Shaban Kissu (Kondoa) na Stephen Zelothe (Musoma).
Wengine ni Pili Moshi (Kwimba); Mahmoud A. Kambona (Simanjiro); Glorius B. Luoga (Tarime); Zainab R. Telack (Sengerema); Bernard Nduta (Masasi); Zuhura Mustafa Ally (Uyui); Paulo Makonda (Kinondoni); Mwajuma Nyiruka (Misungwi) na na Maftah Ally Mohamed (Serengeti).
Wakuu wa Wilaya saba ambao uteuzi wao umetenguliwa lakini watapangiwa kazi nyingine ni Brig. Jenerali Cosmas Kayombo aliyekuwa Simanjiro; Kanali Ngemela E. Lubinga (aliyekuwa Mlele); Juma S. Madaha (aliyekuwa Ludewa); Mercy E. Silla (aliyekuwa Mkuranga); Ahmed R. Kipozi (aliyekuwa Bagamoyo); Mrisho Gambo (aliyekuwa Korogwe) na Elinas A. Pallangyo (aliyekuwa Rombo).
Waziri Mkuu pia aliwataja Wakuu wa Wilaya 12 ambao uteuzi wao umetenguliwa kutokana na sababu za umri, kiafya na kuimarisha utendaji Serikaini na wilaya zao kwenye mabano kuwa ni James K. Ole Millya (Longido); Elias Wawa Lali (Ngorongoro); Alfred Ernest Msovella (Kongwa); Danhi Beatus Makanga (Kasulu); Fatma Losindilo Kimario (Kisarawe); Elibariki E. Kingu (Igunga); Dk. Leticia Moses Warioba (Iringa); Evarista N. Kalalu (Mufindi); Abihudi M. Saideya (Momba); Martha J. Umbulla (Kiteto); Khalid J. Mandia (Babati) na Elias Goroi (Rorya).
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
DODOMA. FEBRUARI 18, 2015.


MWANA FA USO KWA USO NA WAZIRI CHIKAWE MAREKANI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akizungumza na mwanamuziki mkongwe wa Bongo Flava nchini Tanzania, Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA jijini Washington DC katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani. Waziri Chikawe yupo nchini humo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani, na kwa upande wa Mwana FA yupo nchini Marekani kwa ajili ya matembezi yake binafsi hata hivyo alienda ubalozini hapo kwa ajili ya kumsalimia Balozi. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia), Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula wakiwa katika picha ya pamoja na mwanamuziki mkongwe wa Bongo Flava, Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA wakati mwanamuziki huyo alipokutana na Waziri huyo jijini Washington DC katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani. Waziri Chikawe yupo nchini humo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani, na kwa upande wa Mwana FA yupo nchini Marekani kwa ajili ya matembezi yake binafsi hata hivyo alienda ubalozini hapo kwa ajili ya kumsalimia Balozi. Kulia ni rafiki wa mwanamuziki huyo ambaye pia ni mfanyabiashara, Swalah Saidi. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


RAIS KIKWETE APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA MALAWI, KUWAIT AFRIKA YA KUSINI NA KENYA

Baliozi mpya wa Malawi nchini Tanzania Mhe. Hawa Ndilowe akiwasilisha kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete hati za Utambulisho ikulu jijini Dar es Salaam Februari 18, 2015. Katikati anayeshuhudia ni Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage Juma.
Balozi Ndilowe akiwa katika picha na Rais Kikwete na kufanya naye mazungumzo baada ya kuwasilisha hati za utambulisho.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Baliozi mpya wa Malawi nchini Tanzania Mhe. Hawa Ndilowemara mara baada ya kuwakilisha hati za Utambulisho.
Balozi mpya wa Kuwaiti nchini Tanzania Mhe.Jasem Ibrahim Al-Najem akiwasilisha kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete hati za utambulisho ikulu jijini Dar es Salaam Februari 18, 2015.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania akiwa katika picha na Rais Dkt.Jakaya Kikwete.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania na Rais Dkt.Jakaya Kikwete.wakiwa katika mazungumzo baada ya kuwasilisha hati za utambulisho.
Balozi Mpya wa Afrika ya Kusini nchini Tanzania Mhe. Thamsanqa Dennis Mseleku akiwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam jana. Katikati anayeshuhudia ni Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage Juma.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na balozi mpya wa Afrika ya Kusini nchini Tanzania Thamsanqa Dennis Mseleku baada ya kuwasilisha hati zake za utambulisho na kufanya naye mazungumzo.
Balozi Mpya wa Kenya nchini Tanzania Mhe. Chirau Ali Mwakwere akiwasilisha Kwa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete hati zake za utambulisho ikulu jijini Dar es Salaam jana. Katikati anayeshuhudia ni Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage Juma.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na balozi mpya wa Kenya nchini Tanzania Chirau Ali Mwakwere wakikumbatiana na kwa furaha muda mfupi baada ya balozi huyo kuwasilisha hati zake za utambulisho ikulu jijini Dar es Salaam jana. (Picha zote na Freddy Maro)

PINDA ANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI IRINGA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Nduli kuanza ziara ya kikazi mkoani Iringa Februari 18, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama ngoma ya kikundi cha Mangala baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Nduli kuanza ziara ya kikazi mkoani Iringa Februari 18, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na viongozi wa mkoa wa Iringa baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Nduli kuanza ziara ya kikazi mkoan Iringa Februari 18, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua maabara ya Chuo Kukuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa wakati alipotembelea Chuo hicho akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa Februari 18, 2015. Kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Profesa Rwekaza Mkadala.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimsikiliza Mtalaamu wa Mifumo ya computer wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa, Ibrahimu Mwahu wakati alipokagua maabara ya chuo hicho akiwa katika zaiara ya mkoa wa Iringa Febtuari 18, 2015. Kulia kwake ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dr. Shukuru Kawambwa.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na viongozi wa mkoa wa Iringa baada ya kupokea taarifa ya mkoa wa Iringa kwenye ikulu ya Iringa Februari 18, 2015. Kushoto ni Mkuu wamkoa wa Iinga , Amina Masenza. Mheshimiwa Pinda yuko katika ziara ya kikazi mkoani Mbeya.


Wednesday, February 18, 2015

ZIARA YA WAZIRI SIMBACHAWENE MTWARA NA LINDI

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara, Alfred Luanda (aliyesimama), akiwasilisha taarifa fupi ya hali ya mmomonyoko wa ardhi uliosababisha mazingira ya hatari kwa Kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Maurel & Prom Tanzania (M&P), kilichopo Mnazi Bay – Mtwara. Wanaosikiliza ni Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa tatu kutoka Kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu (katikati), na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Nishati na Madini walioongozana na Waziri.
Baadhi ya nyumba wanazoishi wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa pili kutoka Kulia) akikagua nyumba za wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara. Pamoja naye ni Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi Kapuulya Musomba (Kushoto – sambamba na Waziri) na Mkuu wa Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud (Kulia kwa Waziri.
Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi Kapuulya Musomba (kushoto), akifafanua jambo kwa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa pili kutoka kushoto) wakati akikagua nyumba za wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara.
Sehemu ya Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, akikagua sehemu ya Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara wakati wa ziara aliyoifanya mwanzoni mwa wiki mkoani humo.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia) akijadili jambo na mmoja wa wasimamizi wa Mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba – Mtwara, wakati wa ziara yake mwanzoni mwa wiki kukagua maendeleo ya Mradi.
.............................................................................
*SIMBACHAWENE aahidi umeme kwa wana-Msimbati
Na Veronica Simba
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene amefanya ziara mkoani Lindi na Mtwara mwanzoni mwa wiki kukagua miradi mbalimbali iliyo chini ya Wizara yake ambapo aliahidi huduma za umeme na maji kwa wananchi mbalimbali.
Akiwa Madimba mkoani Mtwara, baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa mtambo wa kuchakata gesi, Waziri Simbachawene alimwagiza Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi Kapuulya Musomba kutoa huduma ya maji safi kwa wananchi wanaozunguka maeneo hayo.
"Kutokana na taarifa yenu, mtakuwa na hifadhi ya maji ya kutosha hapa. Pamoja na matumizi yenu mbalimbali, hakikisheni mnatoa huduma ya maji kwa wananchi wanaozunguka mtambo," alisema Waziri.
Vilevile, Waziri Simbachawene alitoa ahadi ya umeme kwa Kijiji cha Luvula kilichoko Msimbati. Alisema Kijiji hicho na vingine 15 vilivyo jirani na Kiwanda cha kufua umeme cha Mnazibay, vitapatiwa umeme kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu.
"Tunaendelea na zoezi la kusambaza umeme nchi nzima. Lengo letu ni kuhakikisha idadi ya watanzania wanaopata umeme inaongezeka zaidi na zaidi ili kuwezesha lengo la nchi yetu kufikia uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kama dira ya maendeleo inavyoonesha," alisema.
Ziara hiyo ya Waziri Simbachawene, ni ya kwanza kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara tangu aliposhika wadhifa wa Uwaziri wa Nishati na Madini, Januari mwaka huu.