Meneja
Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akifafanua bei za
king'amuzi hicho kipya ambapo kwa wateja wapya watajipatia kwa ofa ya
Tsh. 99,000/ kuanzia jana hadi siku Jumapili kilele cha fainali za
michuano ya AFCON huku ambao ni wateja tayari wanabadilishiwa kwa
gharama ya Tshs. 39,000/ ambayo pia ni ofa. Ving'amuzi hivyo vipya vya
DStv HD vinapatikana kupitia mawakala wote wa DStv Tanzania nzima.
Katika
hatua nyingine, DStv wamezindua huduma mpya kwa wateja wao
waliounganishwa na ving'amuzi hivyo vya DStv kuweza kuendelea kufurahia
huduma hiyo kupitia simu zao za viganjani zenye uwezo wa 'Android',
Kompyuta mpakato (Laptop), Tablet, na vifaa vingine vyenye uwezo wa
kupokea usajili wa 'App'.
Akielezea,
juu ya huduma hiyo, Ronald Shelukindo, alibainisha kuwa, kinachotakiwa
ni kwa mteja wa DStv, kwenda kwenye simu yake au Laptop, ama Tablet na
kisha kujisajili kupitia 'App' kwa kujisajili kwa kuandika 'DStv Now'.
Aidha,
Ronald Shelukindo alisisitiza kuwa, huduma hiyo ya DStv Now ni kwa
wateja waliouganishwa na ving'amuzi hivyo tu ambapo wataifurahia huduma
hiyo kwa kuendelea kuangalia chaneli zaidi ya 12 za DStv, ikiwemo ya
Super Sport 3, za filamu, na nyinginezo mbalimbali.
Pia kwa maelezo zaidi wateja wanaweza kutembelea tovuti ya DStv.com |
No comments:
Post a Comment