Timu ya Ivory Coast imefuzu kucheza
fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON, baada ya kuirarua Jamhuri
ya Kidemokrasi ya Congo 3-1 katika nusu fainali ya kwanza iliyochezwa
Jumatano usiku katika mji wa Bata.
Alikuwa nahodha wa Ivory Coast
Yaya Toure aliyeanza kuwanyanyua mashabiki wa Ivory Coast alipofunga
goli katika dakika ya 20 kutokana na mkwaju mkali na kumwaacha mlinda
mlago wa DR Congo, Kidiaba, asijue la kufanya.
DR Congo walisawazisha bao hilo katika dakika ya 24 ya mchezo kwa njia ya penati likifungwa na Mbokani Bezua.
Gervinho akafunga bao la pili katika dakika ya 41. Hivyo hadi mapumziko Ivory Coast ilikuwa mbele kwa mabao 2-1.
Kipindi
cha pili timu hizo ziliendelea kushambuliana. Wilfried Kanon
alikamilisha sherehe kwa timu yake ya Ivory Coast alipofunga bao la tatu
katika dakika ya 68. Kwa matokeo hayo Ivory Coast imetinga fainali za
michuano ya Afcon mwaka 2015, ambapo inamsubiri mshindi wa nusu fainali
ya pili, kati ya Ghana na wenyeji Equatorial Guinea, Alhamisi. Chanzo ni BBCSwahili. |
No comments:
Post a Comment