Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini,Dk. Charles Msonde akizungumza na wanahabari jijini Dar jana.
Shule za sekondari za binafsi zaongoza 10 bora matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Katibu
Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini (NECTA), Dk.Charles Msonde
amesema katika matokeo ya kidato cha nne ya mtihani wa mwaka jana ufaulu
umeongezeka kwa asilimia 12.67 ikilinganishwa na mwaka 2013.
Katika
matokeo hayo msichana wa shule ya sekondari ya Baobab, Nyakaho I.
Marungu ndio aliyeongoza mtihani huo na kufatia wavulana.
Shule za
Sekondari za St.Fransis ya mkoani Mbeya wanafunzi sita na Feza wanafunzi
nane na kufanya shule hizo kuingia katika 10 bora kwa kutoa idadi
wanafunzi wengi ikilinganishwa na shule zingine.
Msonde amasema matokeo hayo yanatokana na mfumo mpya wa GPA kwa kuangalia masomo saba hivyo ufaulu umetokana na mfumo huo. |
No comments:
Post a Comment