Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama akijibu swali Mbunge Bungeni.
Na Lorietha Laurence-Maelezo , Dodoma SERIKALI
kupitia mradi wa uendelezaji miji (TSCP) imefanikiwa kujenga barabara
zenye urefu wa kilometa 42 kwa mji wa Dodoma kwa msaada wa mfuko wa
Benki ya Dunia.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama
ameeleza hayo Bungeni Dodoma, kuwa ujenzi huo wa barabara umehusisha pia
ujenzi wa mifumo ya maji ya mvua, dampo la kisasa kwa Kijiji cha
Chidaya pamoja na mitambo ya usombaji taka.
"Maboresho
hayo ya miundombinu kwa mji wa Dodoma, ni kuhakikisha kuwa mji mkuu huu
wa Tanzania unakuwa katika madhari mazuri na yenye kukidhi haja za
wananchi wake", alisema Waziri Mhagama.
Alizitaja
barabara hizo kuwa ni pamoja na maboresho ya barabara ya Mwanza,
Barabara ya 6 hadi 11,Barabara za Nkuhungu na Chamwino-chang'ombe zenye
jumla ya kilomita 15.7 ambapo ujenzi umekamilika kwa asilimia 100.
Aidha
aliongeza kuwa jumla ya kilomita 27.12 za barabara za pembezoni mwa mji
nazo zilijengwa kwa kiwango cha lami ambazo ni Area A kilomita 5.82,
Kikuyu kilomita 5.65,Kisasa kilometa 12.90 na Chamwino kilometa 2,75.
Hata
hivyo, alisema Benki ya Dunia imeahidi kutoa Dola za Kimarekani milioni
7.66 kwa ajili ya kukamilisha mapungufu yaliyojitokeza katika awamu ya
kwanza kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Independence na barabara ya
mbeya kuelekea uhindini.
|
No comments:
Post a Comment