DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Friday, February 20, 2015

KIGOGO CCM AFARIKI GAFLA MKUTANONI

Mwakilishi wa jimbo la Magomeni, Salmin Awadhi Salmin (pichani) amefariki dunia ghafla jana mchana akiwa mkutanoni katika Ofisi Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui Zanzibar.

Salmin Awadh ambaye pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM  na Mnadhimu wa wajumbe wa CCM Baraza la Wawakilishi Zanzibar amefariki wakati akihudhuria vikao vya chama.

Marehemu Awadh alikimbizwa kwa matibabu katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa uchunguzi zaidi. 
Aidha, taarifa kutoka Ofisi ya Katibu wa Baraza la Wawakilishi, iliyotolewa kwa waandishi wa habari kupitia kwa Mkuu wa Idara ya Utawala, Amour Mohamed Amour imesema mwili wa marehemu utaagwa leo saa 5 asubhi katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi na baadae maziko yatakayo fanyika makunduchi.
Dom Land Blog inatoa pole kwa Wana Magomeni, Familia ya Marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na Wazanzibar wote kufuatia msiba huo mzito.

No comments:

Post a Comment