Kwenye Power Breakfast FEB 2015, Mkurugenzi wa Clouds FM
amesikika live kutoka Dubai, yako mengi kayazungumza, FIESTA2015,
wasanii wa TZ, ishu ya dawa za kulevya, UCHAGUZI 2015 na stori ya Clouds
kuuzwa.
Kwanza kuhusu mipango ya Clouds kusikika nchi nzima; “Kwanza
nimshukuru sana mwenyezi MUNGU. Kwa yale yote ambayo tuliyaomba na
kuwekeza jitihada zetu yametimia, tulikuwa tumebakiza Nachingwea,
Kasulu, Simiyu, Geita, Katavi na Njombe… Hiyo Mikoa tumeimilisha that
means tumekamilisha kuipiga TANZANIA nzima kama tulivyoahidi mwaka jana“
“Sasa
hivi tumejaribu kwa kiasi kikubwa sana kuona tunakwenda kwenye upande wa
digital zaidi, kuingia kwenye mitandao.. tuna-launch Tanzania Box,
Tanzania na dunia nzima watapata nafasi hiyo ya kuweza kuona the biggest
OTT in Tanzania. Mtanzania yoyote leo ukiwa na nafasi ukiingia kwenye
www.tanzaniabox.com utaona content yote ambayo iko humo ndani“
Fiesta 2015 ipo?; “FIESTA
ni sherehe kubwa ya burudani.. Fiesta mwaka huu IPO.. iko palepale na
tumeipanua zaidi kujaribu kunyanyua utamaduni wa KITANZANIA, vyakula vya
kitanzania pamoja na kuipeleka kimataifa zaidi. Ilikuwa tuanze mwaka
huu kutoka kwenda kwenye nchi nyingine lakini nafikiria tutaanza kutoka
mwaka kesho.. FIESTA iko palepale na nafikiria itakuwa ni bora kuliko
miaka yote FIESTA ya mwaka huu..“
Kingine ni kuhusu kufanya show nyingine kubwa ya kumleta msanii mkubwa mbali na Fiesta; “Tuko
katika mazungumzo mazuri kidogo na wasanii wawili watatu ni mapema
kuyazungumza, nafikiria kutakuwa na tamasha lingine zaidi ya ambalo
litainvolve wasanii wakubwa.. Kuna tamasha lingine litakuja mapema sana
pamoja na tamasha la utamaduni“
Dubai ni sehemu ambayo ina connection kubwa, hapa anazungumzia ishu ya kuwapeleka wasanii wa Watanzania; “Tuko
katika mazungumzo na Diamond pamoja na wasanii wawili wadogo,
tunachotaka kufanya ni kuhakikisha wasanii wa Tanzania wakubwa
wanawabeba vilevile wasanii wadogo.. Diamond ni shahidi tuko katika
mazungumzo ya mwisho ili aweze kuja na wasanii wengine either wa kati au
wadogo ili waweze kuwapandisha na wale wadogo wapande..“
Kuhusu Uchaguzi Mkuu 2015; “Ni
watanzania sisi wenyewe ndio wenyewe jukumu kubwa sana kwanza
kujiandikisha kupiga kura and then kuhakikisha kwamba kila Mtanzania
anamchagua mtu ambaye kiukweli atampeleka kutoka kwenye level moja
kwenda nyingine..“
Hapa anaongelea Clouds kuhusishwa na Chama chama cha CCM; “Nimeona
kwenye mitandao, yamezungumzwa mengi kuhusu Clouds kuwa radio ya chama
tawala CCM.. Mimi mwenyewe sina chama, niko neutral.. Kama kuna
individual mmoja au wawili ambao ni mashabiki sio policy ya kampuni..
haturuhusu sisi. Freeman Mbowe ni rafiki yangu wa damu tunafahamiana
miaka mingi zaidi ya miaka 30 kwa nini nisimpe nafasi yeye kama
naendekeza chama“
Kumekuwa na ishu ya mauaji ya albino, hapa anaongelea hilo; “Nimeona
juzi mtoto mdogo wametoa mikono, miguu nchi inakwenda wapi sasa? Watu
wanafikiria maendeleo ni kuuana tena kwa vitu ambavyo havipo. Lazima
nchi nzima sasa hivi tuseme kwamba hiyo kitu tunaipiga vita vibaya sana
na nafikiria Hashtag inayosema #MimiNitakulinda ingeanza kutumika kwa
Watanzania wote sasa hivi na kuhakikisha tunapigana vita kuokoa viumbe
ambavyo kiukweli havina hatia“
Kesi ya dawa za kulevya na wasanii na vijana TZ; “Madawa
ya kulevya ni kitu hatari sana.. imewaona watu wengi ambao nimewajua
kwa muda mrefu wakiteketea.. Ukiingia umeingia kwenye shimo ambalo
hutaweza kuokolewa.. hii vita inatakiwa ipiganiwe na kila mtu. Hawa watu
wanaoharibu watoto wetu kwanini wasifuatiliwe? Tunakwenda kuchagua
viongozi, lazima tuwe sober na tuwe clean kuanzia sasa mpaka
tunapokwenda kuchagua.. #Tanzania2015NoDrugs. Wasanii wangeweza kuwa
pamoja na kampeni hizi ingeweza sana kusaidia nchi yetu“
Zimeenea stori mitandaoni kuhusu Clouds kuuzwa, hapa anajibu kuhusu hilo; “Clouds
imejengwa kwa jasho la kuanzia chini.. Hao wakurugenzi watataka kuuza
leo baada ya kuhangaika miaka yote 15? It’s impossible, hizo habari
hazina ukweli wowote. Sio kampuni moja au mbili au tatu zimetaka
kuinunua Clouds, lakini hatujawa tayari tumejitosheleza na tunaweza
kuendelea wenyewe bado" CHANZO: millardayo.com |
No comments:
Post a Comment