Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias
Chikawe (wapili kulia), Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico,
Liberata Mulamula wakiwa katika picha ya pamoja na mwanamuziki mkongwe
wa Bongo Flava, Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA wakati mwanamuziki
huyo alipokutana na Waziri huyo jijini Washington DC katika Ubalozi wa
Tanzania nchini Marekani. Waziri Chikawe yupo nchini humo kwa ajili ya
kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani,
na kwa upande wa Mwana FA yupo nchini Marekani kwa ajili ya matembezi
yake binafsi hata hivyo alienda ubalozini hapo kwa ajili ya kumsalimia
Balozi. Kulia ni rafiki wa mwanamuziki huyo ambaye pia ni
mfanyabiashara, Swalah Saidi. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi. |
No comments:
Post a Comment