Umati wa mashabiki wakipagawa na Jahazi Modern Taarab.
KUNDI linalotikisa
kunako miondoko ya Pwani, Jahazi Modern Taarab likiongozwa na Mfalme
Mzee Yusuf jana limefunika ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live
katika shoo maalum ya Usiku wa Wapendanao 'Valentine's Day'.
Jahazi
walianza kutawala jukwaa ambapo, Leila alikuwa wa kwanza kupanda na
kuimba Wimbo wa Fanya Yako kisha akafuatiwa na Mwansiti na Fatuma Nyoro.
Baadaye alipanda Mzee Yusuf kwa Wimbo wa My Valentine na kufanya ukumbi
wote kulipuka kwa shangwe. Mzee Yusuf aliamsha shangwe zaidi baada ya
kuimba Wimbo mpya wa Mahaba Niue. |
No comments:
Post a Comment