MARAIS WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUKUTANA NAIROBI, KENYA
Bendera ya Jumuia ya Afrika Mashariki
Marais wa
nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanakutana leo mjini
Nairobi, Kenya baada ya kutofanyika mkutano wa awali uliokuwa umepangwa
kufanyika mwezi Disemba, 2014 mwaka jana mjini Nairobi.
Marais wote watano wa nchi wanachama wanatarajiwa kuhudhuria.
Katika
mkutano huo Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania anatarajiwa kukabidhiwa
Uenyekiti wa Jumuia hiyo kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya,
wadhifa ambao alikuwa akabidhiwe mwezi Disemba, 2014, lakini
hakuweza kuhudhuria mkutano huo kutokana na kwenda kutibiwa nchini
Marekani.
Marais wengine wa nchi wanachama wa Jumuia
ya Afrika Mashariki ni Yoweri Museveni wa Uganda, Paul Kagame wa Rwanda,
Pierre Nkurunzinza wa Burundi, na mwenyeji wa
mkutano Uhuru Kenyatta wa Kenya.
Mbali na
masuala ya uhusiano wa kiuchumi, kisiasa na kijamii miongoni mwa mataifa
hayo, kujadiliwa katika kikao hicho, pia maombi ya nchi za Sudan Kusini
na Somalia kuwa uanachama wa jumuia ya Afrika Mashariki yatajadiliwa. CHANZO: BBC
No comments:
Post a Comment