Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias
Chikawe (wapili kushoto-mstari wa pili), Balozi wa Tanzania nchini
Marekani na Mexico, Liberata Mulamula (nyuma ya waziri) wakimsikiliza
kwa makini Rais Barack Obama (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa
hotuba yake katika Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi
duniani uliofanyika katika Ukumbi wa Loy Henderson wa Wizara ya Mambo
ya Nje, jijini Washington DC nchini humo leo. Mkutano huo
uliowashirikisha Mawaziri wanaoshughulika na masuala ya usalama kutoka
mataifa mbalimbali duniani, Maafisa Waandamizi wa Umoja wa Mataifa (UN),
Vyama vya Kiraia na Sekta Binafsi ulijadili masuala mbalimbali ya jinsi
ya kupambana na vurugu na ugaidi dunaini. Katika hotuba yake, Obama
alisema mapambano dhidi ya watu wenye msimamo mkali hayawezi
kulinganishwa na mapambano dhidi ya waislamu, hivyo hakuna dini yoyote
inayowajibika kwa ugaidi, isipokuwa watu ndio wanaowajibika kwa vurugu
na ugaidi. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi. |
No comments:
Post a Comment