Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini tukio zima lililotoa taarifa sahihi juu ya tatizo la kutoonekana vizuri kwa chaneli za ITV na EATV katika king’amuzi cha kampuni hiyo. Katika mkutano huo Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano nchini, TCRA na StarTimes walitoa ufafanuzi juu ya tatizo linalopelekea tatizo hilo.
……………………………………………………………………….
Taarifa kwa vyombo vya habari
TCRA na StarTimes watoa ufafanuzi kutoonekana vizuri kwa ITV na EATV
Mamlaka
ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kampuni ya matangazo ya
dijitali ya Star Media (Tanzania) Limited wametoa ufafanuzi juu ya
matangazo hafifu ya chaneli za ITV na EATV yalianzakuruka kwa wiki moja
iliyopita.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mkurugenzi Msaidizi wa Ufundi, Kitengo cha
Tekinolojia wa kampuni ya Star Media Tanzania ambao ni wasambazaji na
wauzaji wa ving’amuzi vya StarTimes nchini, Mhandisi Abdulkadir Mbeo
amesema kuwa, “Wakazi wa Dar es Salaam wamekuwa wakipata tabu kutazama
chaneli za ITV na EATV kupitia king’amuzi cha StarTimes kutokana na
muingiliano unaosababishwa na mitambo ya masafa ya WiMAX, tatizo hilo
lililojitokeza mapema mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu. Hali hii
imesababisha usumbufu mkubwa kwa wateja wetu na umma kwa ujumla ambao
wamekuwa wakifurahia matangazo yetu tunayoyatoa katika ubora wa hali ya
juu.”
“Baada
ya uchunguzi wa kutosha uliofanywa na wahandisi kutoka StarTimes kwenye
mitambo yao wamegundua kwamba tatizo limejitokeza katika vyanzo vya nje
ambavyo ni mitambo ya mawasiliano yenye mfumo wa WiMAX.” Alisema na
kuongezea Mhandisi Mbeo, “TCRA kama chombo chenye dhamana ya udhibiti na
urushaji wa matangazo ya dijitali nchini ndio chombo pekee kwa ajili ya
usuluhishi pindi yanapotokea matatizo kama haya ya kuingiliana kwa
mawimbi kwa kampuni zinazohusika.”
“Baada
ya kuwasilisha tatizo hilo, timu ya wahandisi wa kampuni ya StarTimes
na TCRA walifanya uchunguzi wa kutosha ili kuweza kubaini mitambo hiyo
ya WiMAX ambayo imekuwa ikiingiliana na urushaji wetu wa matangazo
katika kituo cha Makongo.” aliongezea
“Utafiti
ulifanyika kwa makini na majibu yakawa mazuri na yenye kuleta ufumbuzi.
Timu iligundua kuwa kuna ufungaji mpya wa mitambo ya WiMAX ambayo
inasababisha muingiliano wa mawimbi ya satelaiti yanayopokelewa na dishi
la stesheni za ITV na EATV na kusababisha upokeo wa mawimbi hafifu
katika dishi linalotumiwa na StarTimes kwenye kituo chake cha kurushia
matangazo.”
“Pili,
timu ya wahandisi hao imebaini kuwa ufungaji huu wa mitambo mipya ya
WiMAX inafanya kazi katika wigo ambao kwenye kiwango cha juu cha
Megahatzi 3.598. Mawimbi hayo yapo karibu na satelaiti ya ITV pamoja na
EATV kwenye kmiwango cha Megahatzi 3.644 na hivyo kusababisha matatizo
ya moja kwa moja kwenye muingiliano wa urukaji wa chaneli hizi. Na
mwisho kabisa, mitambo hii ya WiMAX inapokea nguvu ambayo ni kubwa na
hivyo kuifanya satelaiti inayorusha matangazo katika mitambo ya Makongo
kuchafuka.”
Kutokana
na utafiti huo na tafakari ya kina, ni wazi kwamba mawimbi ya WiMAX
yaliyogunduliwa katika mitambo ya kurushia matangazo ya runinga kwa njia
ya antenna za nje katika kituo cha Makongo inaingiliana na ile ya
satelaiti inayorusha chaneli za ITV na EATV na hivyo kupelekea matangazo
hayo kuchafuka.
“Lakini
katika hali isiyo ya kawaida na bila ya kufanya uchunguzi wa kutosha na
kwa kushirikisha uongozi wa StarTimes, stesheni za ITV na Radio One
zimetangaza kuwa matatizo hayo yamesababishwa kwa makusudi na kampuni
hiyo. Kutoka na taarifa hizo zilizokuwa zikirushwa na vituo vya ITV na
Radio One, wateja wetu na watanzania kwa ujumla wamekumbwa na wasiwasi
na hofu kubwa juu ya utoaji wa huduma zetu.” Alihitimisha injinia wa
kampuni hiyo
Akiongezea
juu ya ufafanuzi huo Mhandisi Masafa wa TCRA, Bw Francis Mihayo
amebainisha kuwa ni kweli wamepokea malalamiko hayo na mpaka sasa
uchunguzi unaendelea ambapo tatizo limekwishagundulika linasubiri
kupatiwa ufumbuzi.
“Ni
kweli tumepokea malalamiko kutoka kwa kampuni ya StarTimes Tanzania
kuwa baadhi ya wateja wao wanalalamika kutoonekana vizuri kwa chaneli za
ITV na EATV jambo ambalo linawaletea usumbufu mkubwa na kupoteza imani
kwao. Sisi kama mamlaka husika na ambao ndio tunadhamana ya kutoa idhini
ya utoaji wa masafa ya urushaji wa matangazo tunaowajibu wa
kushirikiana na pande zote mbili ili kulitatua hili tatizo.” Alisema Bw
Mihayo
“Ningependa
kuwatoa hofu watanzania kuwa uonekaji huo mbovu wa matangazo ya chaneli
hizo sio wa makusudi kama inadhaniwa au kutangazwa kwenu bali ni sababu
za maingiliano ya mitambo ambayo hivi punde tutairekebisha. Nawaomba
muwe na subira kwani lengo ni kuhakikisha kila mtanzania anapata
matangazo bora kabisa ya kidijitali.” Alihitimisha mhandisi huyo kutoka
TCRA.
Naye
kwa upande wake Meneja wa Mauzo wa kampuni hiyo, Bw David Kisaka
alibainisha kuwa, “Tunapenda kuwatoa hofu wateja wetu na watanzania kuwa
StarTimes inongozwa na falsafa makini inayolengwa kumuwezesha kila
mtanzania kuweza kupata matangazo ya dijitali kwa gharama nafuu. Hilo ni
dhahiri kwani mpaka sasa hatuna mpinzani kwa utoaji wa huduma bora za
gharama nafuu zinazopendwa na kila mtu.”
“Hivi
karibuni StarTimes imezindua ofa kabambe ya king’amuzi nafuu cha
kulipia kwa mwezi cha shilingi elfu nne pamoja na kifurushi kipya cha
NYOTA. Huduma hii mpya imewalenga wateja wote hasa wale wa kipato cha
chini ambao siku zote wamekuwa wakiamini matangazo ya dijitali ni kwa
watu wenye vipato vikubwa.” Aliongezea Kisaka
Bw
Kisaka alihitimisha kwa kusema kuwa StarTimes inapenda kuwahakikishia
kuwa siku zite imejidhatiti katika kutoa huduma bora za matangazo ya
dijitali na kwa bei nafuu. Kwa kulifanikisha hilo, kampuni inafanya
jitihada za kutosha kufungua matawi ya kutosha nchi nzima ili kumfikia
kila mtanzania.
|
No comments:
Post a Comment