Wananchi wa Tarafa ya Pawaga, Iringa wakimsikiiza Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
WAZIRI
Mkuu Mizengo Pinda amewataka watanzania hasa wana Chama wa cha Mapinduzi
( CCM) kuwa na subira katika kumpata mwanachama atakayefaa kusimama
kugombea urais kupitia CCM mwaka huu.
Kuwa
tayari wengi sana wamejitangaza wazi wazi na wengine wamejitangaza kimya
kimya kutaka kugombea Urais na kuwa yote heri ila chama kina utaratibu
wake.
" Itafika
wakati ambao kila chama kitasema huyu ndie mtu wetu ambae atapambana na
vyama vingine...tunachosema sisi huyo atakayependekezwa ndie atakuwa
mgombea wetu" alisema Waziri Pinda.
Waziri
Pinda alitoa kauli hiyo leo wakati akiwahutubia wakazi wa Tarafa ya
Pawaga baada ya kuzindua skimu ya umwagiliji itakayowanufaisha wakazi wa
vijiji vitatu kikiwemo cha Magozi, Ilolompya na Mkombilenga uliogharimu
zaidi ya shilingi bilioni 1.6 fedha kutoka kwa wahisani na serikali.
Alisema
kuwa utaratibu wa ndani ya chama anbacho wao ni watawala na wanaoendelea
kuyafanya maendeleo yanaonekana watalazimika kumuunga mkono
atakayeteuliwa na wale wote ambao hawajateuliwa watamuunga mkono
atakayeteuliwa kwa makundi yote kuvunjwa na kuwa na Kundi moja pekee.
Kuwa baada ya mgombea wa chama tawala kupatikana jukumu kubwa ni kuwaomba wapenzi wao wote kumchagua huyo aliyeteuliwa na chama.
Hivyo, Pinda aliwataka wananchi kote nchini kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Alisema
kuwa zoezi hilo ambalo litawahusu wale wote wenye miaka kuanzia 18 na
kuendelea linatarajia kuanza mwezi huu katika Mkoa wa Njombe na kuwa
kila kata zoezi hilo litadumu kwa muda wa wiki mbili ama tatu .
"Nawaombeni
kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na pia kuipigia kura katiba
inayopendekezwa muda ukifika sisi tunaamini ni katiba bora ambayo
imegusa makundi yote yakiwemo ya wafugaji na wakulima pamoja na makundi
mengine"
Kuwa wapo wapotoshaji ambao watafika na kuwadanganya juu ya katiba hiyo inayopendekezwa na wasiwasikilize.
Alisema
kazi kubwa imefanyika katika kuandaa katiba hiyo inayopendekezwa mbali
ya wao (UKAWA) kutoka nje wakati wa bunge hilo la katiba lakini wajumbe
waliobaki walifanya kazi nzuri ya kuandaa katiba hiyo inayopendekezwa
hivyo kuwaomba wananchi kuipigia kura.
Katika
hatua nyingine Waziri Mkuu Pinda amewataka wakulima wa Mpunga Pawaga
katika kuepuka na migogoro kati yao na wafugaji kuweka utaratibu wa
kukusanya majani ya Mpunga na kuyapeleka majumbani kwao ili wafugaji
wapate kununua kuliko kuyaacha mashambani na kuwafanya wafugaji kuingiza
mifugo yao mashambani.
|
No comments:
Post a Comment