DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Monday, February 02, 2015

WASTARA ALA SHAVU

MKALI wa sinema za Kibongo, Wastara Juma amepata shavu la kuwa balozi wa kampeni ya kumsomesha mtoto wa kike ijulikanayo kama Morogoro Education Development Organization (MEDO).
Mkali wa sinema za Kibongo, Wastara Juma akisaini mkataba wa kuwa balozi wa kampeni ya MEDO.
Hafla fupi ya kusimikwa ubalozi huo na kusaini mkataba, ilifanyika hivi karibuni katika Ukumbi wa Hoteli ya Tamal, Mwenge jijini Dar ambapo baada ya kusaini, Wastara alianza kazi rasmi ya kuhamasisha watu kuchangia elimu ya mtoto wa kike huku akiongozwa na kauli mbiu ya kampeni hiyo isemayo 'Sh. 500 yatosha kunipa elimu.'
Wastara Juma akipiga picha ya pamoja na wadau wa kampeni hiyo.
Wastara alishukuru kupewa nafasi hiyo akieleza kuwa ni bahati kwake kwani wasanii wapo wengi.
"Ninawashukuru MEDO kwa kunipa nafasi hii, niwaahidi kuwa nitaitendea haki kuhakikisha nahamasisha uchangiaji wa fedha kwa ajili ya elimu ya watoto wa kike," alisema Wastara. Picha kwa hisani ya Globalpublishers.

No comments:

Post a Comment