MSANII wa
muziki wa Bongo Fleva, Omary Nyembo 'Ommy Dimpoz', amesema anashangazwa
na uvumi unaoendelea kuwa yupo katika uhusiano na mwigizaji wa filamu,
Wema Sepetu. Akielezea kuhusu
picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Ommy Dimpoz, alisema
walikuwa Afrika Kusini kwa mapumziko ndipo picha hizo zilipopigwa. "Tunapiga
picha nyingi sana na Wema, hii siyo mara ya kwanza, lakini sijui
kwanini hizi zimetengeneza taswira nyingine kwa mashabiki," alisema. Picha
za wawili hao wakiwa katika pozi tofauti zimeendelea kuwa gumzo na
kuzua maswali mengi kwa mashabiki, kutokana na ukaribu alionao Ommy
Dimpoz na aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Nasib abdul 'Diamond', Wema Sepetu. CHANZO: MTANZANIA |
No comments:
Post a Comment