Mez B enzi za uhai wake. Moja ya taarifa ya kushtua na kuhuzunisha
zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii, pamoja na watu kutumiana message
ni kuhusu msiba wa aliyekuwa staa wa muziki wa Bongo Fleva, Mez B. Katika
kipindi cha LEO TENA cha Clouds FM wametafutwa watu wa karibu ili kuthibitisha taarifa
hiyo.
Dada wa marehemu ambaye jina lake ni Rachel amethibitisha kuwa msanii MEZ B amefariki akiwa nyumbani kwao Dodoma.
Noorah ni msanii ambaye walikuwa karibu na Mez B,
amesema Mez B alikuwa na homa tangu mwezi December mwaka jana na
baadaye akasafiri kwenda Dodoma huku hali yake ikiwa bado sio nzuri,
mara ya mwisho wameongea kwenye simu ni siku tano zilizopita, leo simu
yake imepokelewa na dada yake akimtaarfu kuwa Mez B amefariki muda mfupi uliopita baada ya kuzidiwa.
Mez B aliwahi kuwa kundi moja Chamber Squad na akina Noorah, Dark Master na marehemu Albert Mangwea pia.
Msiba uko nyumbani kwao eneo la Kisasa, Dodoma. CHANZO: millardayo.com
|
No comments:
Post a Comment