Timu
ya Yanga jana imepaa kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuibanjua Prison ya
Mbeya katika uwanja wake wa nyumbani wa Sokine kwa mabao 3-0.
Mabao ya yanga yalifungwa na wajuzi wale wale walioibanjua katika mchezo wa awali jijini Dar es Salaam iliposhinda mabao 2-1.
Magoli
ya Yanga yamefungwa katika kipindi cha kwanza na Simon Msuva
aliyepachika wavuni goli la kwanza na la tatu huku Andrey Coutinho
akifunga goli la pili.
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1, ambapo bao
la kwanza la Yanga lilifungwa na Andrey Coutinho dakika ya 38,
bao la pili lilifungwa na Simon Msuva katika dakika ya 69, huku bao la
Prisons likifungwa na Ibrahim Kahaka, katika dakika ya 67.
Ushindi huo umeifanya Yanga kufikisha pointi 48 dhidi ya Azam FC yenye pointi 46 ambayo imelazimishwa sare 0-0 katika
mchezo uliopigwa uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
|
No comments:
Post a Comment