Mbunge la Mbunge wa Rombo Joseph Selasini, akiuliza swali.
Naibu
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Anna Kilango Malecela ametoa wito
kwa wamiliki wote wa shule binafsi pamoja na za serikali kuzingatia
kiwango cha ufaulu kutoka kidato kimoja kwenda kingine kilichowekwa na
serikali.
Akijibu
swali la Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini, bungeni mjini Dodoma
aliyetaka kujua kama Serikali inajua na kuunga mkono kiwango cha ufaulu
kwa shule zisizo za Serikali zinazoweka viwango maalum vya ufaulu
tofauti na vile ilivyoviweka.
Naibu
Waziri Anne Kilango alisenma Serikali haiungi mkono utaratibu huo kwa
kuwa umekiuka waraka wa elimu namba 12 wa mwaka 2011 na waraka Namba 4
wa mwaka 2012.
"Napenda
kusisitiza kuwa yeyote atakayekaidi maelekezo haya ya serikali
atachukuliwa hatua kali za kinidhamu kwa mujibu wa sheria ya elimu Namba
25 sura ya 353 kifungu cha 35" alisema Kilango Aliongeza
kuwa Waraka wa Elimu Na. 6 wa mwaka 2011 umetoa maelekezo kuhusu
wastani wa ufaulu katika mtihani wa Kitaifa wa kidato cha pili ambao ni
asilimia 30.
Hivyo
aliwataka walimu waelewe kuwa wanafunzi wanatofautiana katika uelewa
hivyo kuweka kiwango kikubwa cha wastani kunasababisha wanafunzi kukosa
fursa ya kuendelea na masoma na hivyo kuanza utaratibu mpya ya kutafuta
shule.
Alibainisha
kuwa Serikali itazindua program ya KKK Februari 7, 2015 ikiwa na nia
madhubuti ya kuboresha elimu kwa shule zote za serikali katika kutoa
elimu bora kwa wananchi. |
No comments:
Post a Comment