Rais Joachim Gauck wa Ujerumani ameambatana na ujumbe mzito wa wafanyabiasha 14 katika ziara yake ya siku tano nchini.
Rais huyo
aliyewasili jana usiku nchini atazungumzia fursa za uwekezaji katika
kilimo, biashara na usarifishaji. Pia kuhusiana na mradi wa uzalishaji
wa mbolea unatakaofanywa baina ya Kampuni ya Ferrostaal GmbH pamoja na
Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC), yenye uwezo wakuzalisha
mbolea tani 1.3 milioni kwa mwaka.
Akitoa
taarifa ya ujio wa rais huyo jana, jijini Dar es Salaam, balozi mdogo wa
Ujerumani nchini, John Reyels alisema baada ya kuwasili, kiongozi huyo
atakuwa na mazungumzo ya faragha na Rais Kikwete ambayo yatalenga mambo
mbalimbali ikiwamo suala la uwekezaji.
Licha ya
kuwa, Balozi Reyels hakufafanua zaidi kuhusiana na kile atakachozungumza
Rais Gauck, lakini alisema kuwa kupitia wajumbe 14 ambayo ni
wafanyabiashara wakubwa wa nchini humo wataangazia fursa za uwekezaji
nchini na mradi huo unaotarajiwa kutekelezwa kati ya 2019/2020.
Wajumbe
hao ni kati ya wajumbe 90 waliyoongozana na Rais Gauck katika ziara yake
nchini ambayo ataifanya kwa siku tano na kurejea Ujerumani.
Rais
huyo, ambaye anatembela Tanzania kwa mara ya kwanza kutokana na mwaliko
wa Rais Kikwete, pia atatembelea Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT), Usharika wa Azania Front.
"Wakati
ziara yake kanisani hapo Rais Gauck atakuwa na mazungumzo na Askofu Mkuu
wa kanisa hilo, Alex Malasusa,"alisema Balozi Reyels.
Balozi
Reyels, alieleza sababu ya Rais huyo kutembelea kanisa hilo na kusema
kuwa, "Kanisa hilo linahistoria kubwa na Ujerumani kwani lilijengwa na
Wajerumani takriban miaka 100 iliyopita. Hata hivyo, Rais mwenyewe
aliwahi kuwa mchungaji kabla ya kuwa na wadhfa alionao sasa" CHANZO: MWANANCHI. |
No comments:
Post a Comment