Waziri wa
Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia) akijadili jambo na mmoja
wa wasimamizi wa Mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba – Mtwara, wakati
wa ziara yake mwanzoni mwa wiki kukagua maendeleo ya Mradi.
.............................................................................
*SIMBACHAWENE aahidi umeme kwa wana-Msimbati Na Veronica Simba Waziri
wa Nishati na Madini, George Simbachawene amefanya ziara mkoani Lindi
na Mtwara mwanzoni mwa wiki kukagua miradi mbalimbali iliyo chini ya
Wizara yake ambapo aliahidi huduma za umeme na maji kwa wananchi
mbalimbali. Akiwa Madimba
mkoani Mtwara, baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa mtambo
wa kuchakata gesi, Waziri Simbachawene alimwagiza Msimamizi Mkuu wa
Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi Kapuulya Musomba kutoa huduma ya maji
safi kwa wananchi wanaozunguka maeneo hayo. "Kutokana
na taarifa yenu, mtakuwa na hifadhi ya maji ya kutosha hapa. Pamoja na
matumizi yenu mbalimbali, hakikisheni mnatoa huduma ya maji kwa wananchi
wanaozunguka mtambo," alisema Waziri. Vilevile,
Waziri Simbachawene alitoa ahadi ya umeme kwa Kijiji cha Luvula
kilichoko Msimbati. Alisema Kijiji hicho na vingine 15 vilivyo jirani na
Kiwanda cha kufua umeme cha Mnazibay, vitapatiwa umeme kabla ya mwezi
Oktoba mwaka huu. "Tunaendelea
na zoezi la kusambaza umeme nchi nzima. Lengo letu ni kuhakikisha idadi
ya watanzania wanaopata umeme inaongezeka zaidi na zaidi ili kuwezesha
lengo la nchi yetu kufikia uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025
kama dira ya maendeleo inavyoonesha," alisema. Ziara
hiyo ya Waziri Simbachawene, ni ya kwanza kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara
tangu aliposhika wadhifa wa Uwaziri wa Nishati na Madini, Januari mwaka
huu. |
No comments:
Post a Comment