Michezo
ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, UEFA ilianza kutimua tena vumbi
Jumanne usiku kwa michezo miwili katika hatua ya kumi na sita bora.
Paris
Saint Germain ya Ufaransa iliwaalika Chelsea ya England, huku Bayern
Munich ya Ujerumani wakiwa wageni wa Shaktar Donetsk ya Ukraine. Matokeo
ni kwamba PSG na Chelsea zimemaliza dakika tisini za mchezo kwa
kufungana bao 1-1.
Chelsea
ndio waliokuwa wa kwanza kutikisa nyavu za wenyeji wao katika dakika ya
36, bao likifungwa na Branislav Ivanovic na kudumu hadi mapumziko. PSG
waliendeleza mashambulizi huku kiungo wake David Luiz akiwadhibiti
wachezaji wa timu yake ya zamani, Chelsea. Kwa David Luiz kutawala
sehemu ya kiungo, mshambuliaji Matuidi wa PSG alikuwa akitamba na
kuelekeza mashambulizi makali langoni mwa Chelsea na kumfanya mlinda
mlango wake Curtois kuokoa michomo mingi. Katika dakika ya 54 ya mchezo,
Edinson Cavani aliisawazishia timu yake bao na hivyo hadi mwamuzi
anapuliza filimbi yake ya mwisho, timu hizo zilitoka sare ya bao1-1.
Bayern
Munich ya Ujerumani katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora
walipomenyana na Shakhtar Donetsk na kutoka sare ya 0-0Nayo Bayern
Munich ya Ujerumani ilishuhudia ikitoka sare ya kutofungana na Shakhtar
Donetsk ya Ukraine. CHANZO: MjengwaBlog |
No comments:
Post a Comment