DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Sunday, February 15, 2015

MEMBE APOKEA HATI ZA ZA UTAMBULISHO ZA MABALOZI WAPYA WA KUWAIT, MALAWI, KENYA NA AFRIKA KUSINI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Kuwait hapa nchini, Mhe. Jasem Ibrahim Al-Najem jana ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa Waziri akipokea zawadi kutoka kwa balozi mpya wa Kuwait hapa nchini mara baada ya kuwasilisha Nakala ya Hati ya Utambulisho.
Mheshimiwa Waziri Bernard Membe akizungumza na Balozi mpya wa Kuwait hapa nchini Mhe. Jasem Ibrahim Al-Najem jana ofisini kwake jijini Dar es Salaam mara baada ya zoezi la kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho kukamilika.
Mazungumzo yakiendelea huku maofisa wa wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahya, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati (kushoto), Bi.Mindi Kasiga, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali (kulia) na Bw. Thobias Makoba, Katibu wa Waziri wakifuatilia kwa makini mazungumzo hayo.
 Balozi mpya wa Kuwait hapa nchini Mhe.Jasem Ibrahim Al-Najem akiwa katika picha ya pamoja na waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe (kulia) pamoja na Mheshimiwa Balozi Hassan Simba Yahya.
Mheshimiwa Waziri Membe akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mpya wa Malawi hapa nchini Mhe. Hawa Ndilowe.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Malawi hapa nchini Mhe. Hawa Ndilowe jana ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Balozi mpya wa Malawi hapa nchini Mhe. Hawa Ndilowe akimsikiliza Mhe. Membe mara baada ya kukabidhi Nakala za Hati za Utambulisho ofisini kwa Waziri jijini Dar es Salaam.
Balozi mpya wa Afrika Kusini hapa nchini Mhe. Thamsanqa Dennis Msekelu akiwasilisha Nalaka za Hati za Utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa Waziri Membe akifanya mazungumzo na Balozi wa Afrika Kusini hapa nchini ofisini kwake muda mfupi baada ya kupokea Nakala za Hati za Utambulisho.
Mheshimiwa Waziri akiwa katika picha ya pamoja na Balozi mpya wa Kenya hapa nchini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Kenya hapa nchini Mhe. Chirau Ali Mwakwere jana ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Kenya hapa Nchini pamoja na Naibu wake wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe baada ya kukabidhi Nakala za Hati za Utambulisho.
 Balozi wa Kenya hapa Nchini pamoja na Naibu wake wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe baada ya kukabidhi Nakala za Hati za Utambulisho, huku afisa wa wizara ya Mambo ya Nje Bi. Zulegha Tambwe akinukuu mambo muhimu katika mazungumzo hayo.

No comments:

Post a Comment