DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Tuesday, December 30, 2014

SAA 24 ZA BURUDANI DAR LIVE


MVUA YALITIKISA JIJI LA DAR



Haya ni mafuriko madogo yaliyotokea jana baada ya mvua kubwa iliyonyesha kwa saa kadhaa maoneo mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam. Mvua hizo zilileta kizaa zaa katika baadhi ya mitaa na barabara jijini kama inavyoonekana pichani. Hapa ni Akiba katika barabara ya Bibi Titi Mohamed.

Barabara ya Bibi Titi eneo la Akiba 
Hii ni Bibi Titi eneo la Gold Star.

Baada ya mvua kubwa ya takriban saa mbili mfululizo, maeneo mengi jijini Dar es salaam yamejaa maji na kusababisha adha kubwa kwa wakazi wa jiji hilo. Pichani ni eneo la barabara ya Morogoro.
Matolori ya kuuzia "Ice Creame" yakiwa yameachwa na wahusika, huku wapita njia wakivuka maji hayo bila ya habari na kiburudisho hicho.

"THE MBONI SHOW" SASA NDANI YA TBC KUANZIA JANUARI 02, 2015

Mkurugenzi wa 'Mboni Show', Mboni Masimba (wa pili kutoka kulia) akizungumza na waandishi wa habari jana katika  ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam wakati akitangaza kuanza kwa msimu wa tatu wa kipindi chake 'The Mboni Show' kinachotarajia kuanza Januari 02, 2015. Kushoto ni Kiti Simpompa na kuanzia kulia ni Afisa Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Magira Werema na Kaimu Mkurugenzi wa Masoko TBC, Bw. Fadhili Chilumba.

Kutoka Kulia Afisa Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Magira Werema akizungumza wakati wa uzinduzi kipindi cha 'The Mboni Show' uliofanyika katika Ukumbi wa Idara Habari Maelezo jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko TBC, Bw.Fadhili Chilumba pamoja na Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba.
 
Na Mwandishi Wetu.
Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba ameamua kuhamishia kipindi cha Mboni show katika kituo cha utangazaji cha Taifa (TBC) kutoka EATV ili kuvutia watazamaji wengi na wapya kwa wazee pamoja na vijana.
Kipindi cha Mboni Show kitaanza kurushwa TBC kuanzia Januari 02 mwaka 2015 siku ya Ijumaa saa 3 usiku hadi saa 4 usiku na marudio Jumanne saa 9:00 alasiri hadi saa 10:00 jioni.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar ndani ya ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Mboni Masimba ametoa shukrani kwa EATV kwa ushirikiano wao kwa kipindi chote alichokuwa nao, na kusema kuwa amehamishia kipindi cha Mboni Show katika kituo cha TBC ili kuvutia watazamaji wengi hakuna atakaye tumia jina la Mboni Show na hakuna kitakachomkwamisha kwa vile ana hati miliki.
“Nimehamia TBC kwa kuwa nahitaji watazamaji wengi, wote wazee na vijana na hakuna atakaye tumia jina langu la Mboni Show kwa kuwa nina hati miliki ya jina hili”alisema Mboni.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Masoko TBC, Bw. Fadhili Chilumba amesema wamefurahi kuwepo kwa Mboni Show katika kituo cha Taifa (TBC) na kutoa wito kwa mashabiki kuweza kuwadhamini watu kama akina Mboni na wanamkaribisha sana.
Nao wadhamini wa Mboni Show, Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Magira Werema wamesema wanamwezesha Mboni kuwepo hewani ili kuhamasisha, kuelimisha pamoja na kuburudisha umma wa Watanzania.

Tuesday, December 23, 2014

AIRTEL YATOA MSAADA KWA WALEMAVU

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba  akikata utepe kama ishara ya kukabidhi vibanda vya kisasa vya Airtel Money kwa watu wenye ulemavu, wanachama wa Taasisi ya Haki za Binadamu na Maendeleo Watu wenye Ulemavu (HREDP), kwa ajili kuwawezesha kuwa wafanyabiashara wajasiriamari, katika hafla iliyofanyika kwenye Shule ya Msingi Buguruni Viziwi jijini Dar es Salaam jana. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya na (kulia) ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Abubakar Rakesh na mnufaika wa kibanda hicho, Hebron Mwansele (kwenye baiskeli).
 Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akikagua kioski baada ya kukabidhi.
 Sehemu wa wanachama wa Taasisi ya Haki za Binadamu na Maendeleo Watu wenye Ulemavu (HREDP), wakiwa katika hafla hiyo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akiwatunza pesa wanamuziki ya walemavu ya Bendi ya Tunawajali, iliyokuwa ikitumbuiza katika hafla hiyo.

UEFA GOO NIGHT CLUB: KUZINDULIWA MKESHA WA KRISMAS





 

Kiwanja kipya cha maraha Uefa Goo Night Club kinatarajiwa kuzinduliwa mkesha wa sikukuu ya Krismas jijini Dar es salaam Kiwanja hiki ni cha Kisasa kiko maeneo ya Ukonga Mombasa Barabara ya kuelekea Moshi Baa Karibu na njia panda ya Mahita mita 200 kutoka barabara kuu iendayo Pugu, siku ya mkesha wa Krismas burudani kibao zimeandaliwa  na kiwanja hicho kiko katika hatua za mwisho mwisho kukamilisha kila kitu ili kuwapa burudani wateja wake ikiwa ni pamoja na Ligi mbalimbali za ulaya, muziki wa kisasa kama vile Bongofleva na muziki wa zamani na vyakula mbalimbali vitapatikana.

DKT. BILAL AZINDUA RASMI MAJENGO YA TAASISI YA MAFUNZO YA UANASHERIA KWA VITENDO NCHINI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa tatu kushoto) akikata utepe kuzindua rasmi Majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania, wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki, kwa pamoja wakifunua kitambaa kuweka Jiwe la Msingi katika Majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania, wakati wa hafla ya uzinduzi wa majengo hayo uliofanyika jana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki, walipoingia katika chumba maalum cha mafunzo ya Uanasheria kwa vitendo wakati wa uzinduzi wa Majengo ya Taasisi hiyo ya  Mafunzo uliofanyika jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akizindua rasmi Majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania, katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam, jana.
Mafunzo kwa Vitendo yakiendelea katika Taasisi hiyo jana.
Baadhi ya Viongozi na wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia, katika uzinduzi huo jana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la viwanja vya Majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania jana.

PINDA AKUTANA NA KIONGOZI WA KAMPUNI YA GESI YA QATAR

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Bw. Otty Msuku ambaye ni Mtanzania, Mtalaamu wa upimaji ardhi katika mradi wa ujenzi wa bandari mpya ya Qatar wakati alipotembelea eneo la ujenzi wa bandari hiyo akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo Desemba 22, 2014. Katikati ni Mkurugenzi mwendeshaji wa Mradi huo, Don Morrison.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda akikaribishwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mradi wa Ujenzi wa Bandari mpya ya Qatar, Bw. Yusuf Ahmad Al Hammadi wakati alipotembelea eneo inapojengwa bandari hiyo kubwa na yakisasa akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo Desemba 22, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Gesi ya Qatar (Qatargas Operating Company Limited), Bw. Khalid Al Thani wakati alipotembelea ofisi kuu ya kampuni hiyo mjini Doha kujifunza uwekezaji wenye maslahi mapana ya taifa katika sekta ya gesi akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo Desemba 22, 2014. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)

JK AMTOSA TIBAIJUKA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete amemuachisha kazi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo  Makazi Prof. Anna Tibaijuka kutokana na tuhuma za kupata mgao wa Fedha za Akaunti ya Escrow kiasi cha bilioni Moja na Milioni Mia Sita ambazo alidai amepewa mchango kwa ajili ya shule, Rais Jakaya amesema tumeamua mwenzetu huyu atupishe ili tuchague mtu mwingine wa kuhudumu katika wizara hiyo kutokana na maswali magumu.
Akiwa kama Mtumishi wa serikali ambaye anatakiwa kufuata maadili ya Utumishi  wa umma  aliamua kupokea kiasi kikubwa cha fedha huku akijua kimaadili kama mtumishi wa serikali haitakiwi, Rais Dkt. Jakaya Kikwete amesema hayo wakati  akizungumza na taifa kupitia Wazee wa Dar es Salaam jana katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wa Wiazara hiyo Eliackhim  Maswi  amesema ameagiza uchunguzi ufanyika na katika muda wa siku mbili au tatu hivi atapewa taarifa ya uchunguzi huo na kuchukua hatua stahiki.
Na Kwa upande wa Majaji wa Mahakama Kuu waliotuhumiwa Rais Dkt. Jakaya Kikwete amesema anamwachia Jaji Mkuu Mhe. Jaji Mohammed Chande Othman ili achukue hatua za kimaadili kutokana na taratibu za kimahamama na mara baada ya kujiridhisha atapewa taarifa na Jaji mkuu na kuchukua hatua.

RC DAR APETA UJENZI WA MAABARA: AMPA RAIS JAKAYA KIKWETE ZAWADI YA MAFANIKIO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick, akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuzungumza na Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo alimpa taarifa Mheshimiwa Rais juu ya mafanikio ya ujenzi wa maabara katika Shule za Sekondari jijini Dar es Salaam kwa asilimia 100 pamoja na matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mkoa wa Dar es salaam kwa asilimia 76 ukiacha mitaa miwili ambayo uchaguzi haukufanyika kwa sababu ya vurugu ambapo wahusika wote wanashughulikiwa kisheria kutokana na vurugu walizosababisha.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam ambao waliitika wito wa kumsikiliza wakati wa kulihutubia Taifa kupitia Wazee kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisoma hotuba yake kwa Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam jana.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Taifa kupitia Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo alizungumzia uchaguzi na kutaka polisi kufanya kazi yao katika kuhakikisha uchaguzi ujao  hauvurugwi na pia alifafanua mambo mbali mbali yaliyokuwa yakizungumziwa kuhusu akaunti ya Tegeta ESCROW na kumwajibisha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipanga vyema karatasi zenye hotuba yake wakati akiwahutubia Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam jana.
 Ukumbi wa Diamond Jubilee ukiwa umefurika Wazee waliokuja kumsikiliza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
 Baadhi ya Wanasiasa wakongwe waliohudhuria.
Rais Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Kinondoni Iddi Azzan muda mfupi baada ya kulihutubia taifa kupitia wazee wa Dar es Salaam jana kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Rais Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mkono wananchi wakati akiwaaga jana mara baada ya kuzungumza na taifa kupitia wazee wa Dar es Salaam (picha na Freddy Maro).

RAIS JACOB ZUMA AKUTANA NA RAIS KIKWETE IKULU

 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini kufanya mazungumzo ikulu jijini Dar es Salaam juzi.

Rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakikagua gwaride la heshima, wakati Rais huyo wa Afrika ya kusini, akiondoka nchini baada ya kumaliza ziara yake ya siku moja.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (kushoto) na Rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma wakifurahia burudani ya ngoma za asili, wakati wakiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Rais Zuma alipokuwa akiondoka baada ya kumaliza ziara yake ya siku moja nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, wakati akiondoka nchini baada ya kumaliza ziara yake ya siku moja.