Kiungo wa timu ya Manchester United
Ander Herrera amesisitiza hajawahi kupanga matokeo ya mechi wakati
akiichezea klabu Real Zaragoza.
Mhispania huyu ametajwa katika
kundi la wanamichezo 41 wakiwemo wachezaji, makocha na wakurugenzi
katika uchunguzi wa kashfa ya upangaji matokeo kwenye ligi kuu ya
Hispania.
Herrera ameandika katika ukurasa wake wa
facebook kuwa: "Sijawahi na kamwe sintofanya chochote katika kupanga
matokeo, naupenda mpira naamini katika mchezo wa haki nje na ndani ya
uwanja" alisema Herrera kinda wa Kihispania mwenye umri wa miaka 25.
Waendesha mashitaka wanadai fedha taslimu € 965,000
zililipwa kwa kocha Javier Aguirre na wachezaji tisa wa Zaragoza, ikiwa
ni pamoja na Herrera, kabla ya mchezo wa La Liga mwishoni mwa msimu wa
2010-2011.
Herrera aliondoka Zaragoza na kujiunga na timu ya
nyumbani kwao ya Athletic Bilbao mwezi Agosti 2011, kabla ya kujiunga na
Man United mwezi Juni 2014. |
No comments:
Post a Comment