DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Saturday, December 20, 2014

KIWANDA CHA SUKARI KAGERA CHAZALISHA ZAIDI

Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakioneshwa kwa vitendo matrekta yanayotumia setalaiti kusawazisha shamba kwa ajili ya uzalishaji miwa.
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakioneshwa mashine ya kumwagilia maji miwa ijulikanayo kwa kitaalamu kama Centre Pivot System.
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikikagua mitambo ya kuzalishia sukari katika Kiwanda cha Sukari cha Kagera.
Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Mwenye kofia ya bluu) akionja sukari inayozalishwa na Kiwanda cha Sukari cha Kagera. Kushoto ni Mratibu wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Senya Tuni.
Meneja wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera, Bw. Ashwin Rana (Kulia) akiwaonesha Wakaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango mashine mpya zinazotumika kuvutia maji kwa ajili ya kumwagilia miwa.
Msimamizi Mkuu wa Mtambo wa maji wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera, Mhandisi Abdul Adinani (Kulia) akitoa maelekezo ya namna ya maji yanavyochujwa kabla ya kutumika kwa ajili ya umwagiliaji wa miwa. Wanaomsikiliza ni Wakaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Mtaalamu wa uchongaji na usawazishaji wa ardhi kwa ajili ya mashamba ya miwa, Mhandisi Ali Khamis (Kulia) akitoa maelezo ya namna matrekta yanayotumia setalaiti (hayapo pichani) yanavyofanya kazi. Wanaomskiliza ni Prof. Longinus Rutasitara (Kushoto) ambaye ni Naibu Katibu Mtendaji anayeshughilikia masuala ya Uchumi Jumla na  Katikati ni Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri.

No comments:

Post a Comment