Majina
ya wanafunzi wa Darasa la Saba 2014 ambao wamefaulu na kuchaguliwa
kujiunga na masomo ya sekondari (Kidato cha Kwanza) mwaka 2015
yanapatikana katika mbao za matangazo katika shule za Msingi walizo soma
watoto hao na katika ubao wa matangazo wa ofisi za Kata zilizopo
jirani.
Hivyo,
wazazi na wanafunzi wametakiwa kufika katika shule husika au katika
Ofisi za Kata kuangalia majina ya wanafunzi hao na shule walizo
chaguliwa. Pichani ni baadhi ya wanafunzi na wazazi wakiangalia majina
hayo katika ofisi ya Mtendaji Kata ya Makurumla jijini Dar es Salaam
juzi.
|
No comments:
Post a Comment