Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete amemuachisha kazi Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo Makazi Prof. Anna Tibaijuka kutokana na tuhuma za kupata
mgao wa Fedha za Akaunti ya Escrow kiasi cha bilioni Moja na Milioni Mia
Sita ambazo alidai amepewa mchango kwa ajili ya shule, Rais Jakaya
amesema tumeamua mwenzetu huyu atupishe ili tuchague mtu mwingine wa
kuhudumu katika wizara hiyo kutokana na maswali magumu.
Akiwa
kama Mtumishi wa serikali ambaye anatakiwa kufuata maadili ya Utumishi
wa umma aliamua kupokea kiasi kikubwa cha fedha huku akijua kimaadili
kama mtumishi wa serikali haitakiwi, Rais Dkt. Jakaya Kikwete amesema
hayo wakati akizungumza na taifa kupitia Wazee wa Dar es Salaam jana
katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Kwa
upande wa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo na
Katibu Mkuu wa Wiazara hiyo Eliackhim Maswi amesema ameagiza uchunguzi
ufanyika na katika muda wa siku mbili au tatu hivi atapewa taarifa ya
uchunguzi huo na kuchukua hatua stahiki.
Na
Kwa upande wa Majaji wa Mahakama Kuu waliotuhumiwa Rais Dkt. Jakaya
Kikwete amesema anamwachia Jaji Mkuu Mhe. Jaji Mohammed Chande Othman ili
achukue hatua za kimaadili kutokana na taratibu za kimahamama na mara
baada ya kujiridhisha atapewa taarifa na Jaji mkuu na kuchukua hatua.
|
No comments:
Post a Comment