Chama cha
vilabu vikubwa vya soka barani ulaya (ECA) wanataka michuano ya Kombe
la Dunia ya mwaka 2022 itakayofanyika nchi Qatar ifanyike kati ya Mei 5
na Juni 4 mwaka huo.
Shirikisho
la soka duniani FIFA walitangaza mwezi uliopita kuwa michezo ya
michuano hiyo itafanyika kati ya Januari na Februari au Novemba na Desemba.
Lakini
mapendekezo yanayotolewa na Chama cha Vilabu Vikubwa vya Soka (ECA) na
wakilishi wa ligi za kulipwa ulaya (EPFL) wanataka mashindano hayo
yacheze mwanzo mwa majira ya joto sababu itakua ndio salama kwa afya za
wachezaji.
Uamuzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Dunia {FIFA} kuhusu wakati gani michuano hiyo ifanyike inatarajiwa kutolewa Machi, 2015.
ECA na
EPF wanaamini pendekezo yao mpya yanaonyesha jinsi mashindano inaweza
kuchezwa Mei na Juni bila kuhatarisha afya za wachezaji na viongozi.
Pia
kufanyika kwa kombe la dunia mwezi mei na juni kutakua hakuna madhara
kwa michuano ya klabu bigwa barani ulaya, michezo ya olimpiki na waumini
wa dini ya kiislam watakua wamemaliza mfungo mtukufu wa Ramadhani. CHANZO: BBC |
No comments:
Post a Comment