DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Tuesday, December 23, 2014

JK ATUNUKU KAMISHENI MAAFISA WA JESHI MONDULI

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi na kumpongeza Luteni Usu Edwin Engelbert Kessy wakati wa hafla ya kutunuku kamisheni maafisa wa jeshi baada kuibuka mwanafunzi bora wakati wa mafunzo ya maafisa wa jeshi yaliyofanyika katika chuo cha jeshi Monduli mjini Arusha hivi karibuni.
Rais Kikwete, akimpongeza afisa huyu wa jeshi.
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Dkt. Jakaya Kikwete, na vingozi wengine wa juu wa serikali na Jeshi la Wananchi Tanzania-JWTZ, wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu hao.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowassa mara baada ya kuwatunuku kamisheni maofisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa cheo cha Luteni Usu, hafra ambayo  ilifanyika katika chuo cha jeshi hilo kilichopo Monduli, mkoani Arusha.
Mhe. Lowasa, akiteta na maafisa wa jeshi, kushoto ni Mkuu wa Majeshi, Jenerali Devis Mwamunyange.
Mhe. Lowasa akiteta jambo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi.
Maafisa wa jeshi wakiwa kwenye gwaride.
Maafisa wahitimu wa mafunzo ya kijeshi, wakitoa heshima kwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Dkt. Jakaya Kikwete (hayupo pichani) wakati wa gwaride la kuhitimu mafunzo hayo hivi karibuni.
Lowasa akiteta jambo na Mkuu wa Majeshi, Jernerali Davis Mwamunyange.
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange, akiteta jambo na Mbunge wa Monduli mkoani Arusha, Mhe. Edward Lowasa. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Tibenda.

No comments:

Post a Comment