Charles Amon Mihayo (36) Mtanzania mwemye makazi ya kudumu anayeishi mjini Melbourne, nchini Austaralia, amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kutiwa hatiani katika kesi ya mauaji iliyokuwa ikimkabili.
Mihayo
alikuwa akikabiliwa na kesi ya mauaji ya kikatili dhidi ya watoto wake
wawili kosa alilolitenda ili kulipiza kisasi kwa mkewe baada ya
kumuacha.
Mihayo
alifanya ukatili huo kwa wanae Savannah (4) na Indianna (3)
Aprili 20, 2014 nyumbani kwake huko Melbourne wakati wakicheza mchezo wa
kujificha na kutafuta vitu wakati wa sherehe ya Pasaka, amehukumiwa jana
kifungo hicho.
Inadaiwa
kuwa baada ya kuachwa na mke wake, hasira zilimfanya bwana Mihayo kuamua
kufanya ukatili wa kukatisha uhai wa watoto wake mwenyewe Savannah (4) na
Indianna (3), ili tu kumuumiza mke wake kama njia ya kumlipizia kisasi.
Inadaiwa kuwa aliwauwa kwa kuwakandamiza na mto baada ya kucheza nao.
Taarifa
hiyo
inaeleza kuwa siku mauaji hayo yalipofanyika, mama wa watoto hao
aliwapeleka kwa baba yao bwana Mihayo, kufuatia ombi la mzazi mwezake
kutaka kuwaona watoto wake hao kwa mara ya mwisho na kuwaaga. Aidha inaelezwa kuwa Mihayo aliwanunulia nguo mpya na viatu watoto wake. Kabla ya
kutenda ukatili huo kwa damu yake mwenyewe, Mihayo aliwarekodi video wakicheza
muziki huku akicheza nao.
Baada ya kuwauwa aliwaogesha na kisha kuwavalisha nguo mpya alizo wanunua na kuwaweka vyema na kuwapigia simu Polisi.
Mtalaka
wake huyo anae ishi mtaa jirani na Mihayo akiwa na mama yake walikaa
jirani na mara zote walisikia watoto wakicheza lakini mara wakaona kimya
kimetawala aliamua kubisha hodi mara kadhaa ndipo Mihayo akamjibu
"Utafahamu
pindi watakapo fika hapa," na kbla ya mtalaka wake huyo kwenda kupiga
simu polisi askari walifika na Mihayo kufungua mlango mkononi akiwa na
taulo na kusema “Tayari, nimewaua. Nimewaua watoto
wangu. Inabidi mumuulize huyu (mama yao) sababu.”.
Awali katika video ambayo polisi baadae waliiona,
alisikika akiwaambia binti zake wamuoneshe mama yao nguo mpya alizowanunulia,
na walifanya hivyo na kisha mwanaume huyo akakaa mbele ya camera na kusema
“tutamuonesha mama kitu kingine dakika kumi zijazo”, na kuendelea kucheza nao
hadi alipowakandamiza na mto (pillow) hadi kufa.
Polisi
waliwakuta watoto hao wakiwa tayari wamefariki huku wakiwa wamevalishwa nguo na
viatu vipya ambavyo walinunuliwa na baba yao siku hiyo.
Hukumu hiyo ya Jaji Lex Lasry wa Mahakam Kuu ya Victoria, itamlazimu Charles Mihayo kutumikia kifungo cha
miaka 31 kabla ya kupata haki ya kupewa msamaha.
|
No comments:
Post a Comment