Usajili wa wachezaji kwa dirisha
dogo nchi kwa msimu wa mwaka 2014/2015 umefugwa rasmi jana
usiku kwa vigogo wa soka Simba, Yanga pamoja na Azam kusajili nyota
wengi wa kigeni
Simba Sc yenye maskani yake mtaa wa msimbazi
wamefanya usajili wa wachezaji Hassan Kessy toka Mtibwa, Dan Sserunkuma, Simon Sserunkuma, na Beki Juuko Murushid toka Uganda na kukamilisha
idadi ya wachezaji watano toka Uganda akiwemo Joseph Owino na
mshambuliaji Emmanuel Okwi.
Kwa upande wa Yanga wamefanya
marekebisho ya kikosi chao kwa kuwasajili Dany Mrwanda ,Kpah Sherman
toka Aries Fc na Amisi Tambwe toka Simba Sc.
Huku mabigwa watetezi
Azam wakiwasajili beki Serge Wawa Pascal kutoka Ivory Coast, aliyekuwa
anacheza El Merreikh ya Sudan na Amri Kiemba aliyekuwa Simba SC, na
winga Brian Majwega toka klabu ya Kcca.
Vinara wa ligi Mtibwa Sugar wamewaongeza kiungo mzoefu Henry Joseph Shindika, na Abdul Jeba toka klabu ya Chuoni ya Zanzibar.
Timu
nyingine zimefanya pia usajili wa kuboresha vikosi vya kabla ya kuanza
kwa mzunguko wa pili wa kuu ya Tanzania bara maarufu kama VPL.
Jumla ya wachezaji 15 wa kigeni wameombewa ITC ili kuweza kuzitumikia timu zao kabla ya raundi ya pili kuanza.
Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya chama cha mpira Tanzanian(TFF)
inatarajia kukutana hivi karibuni kwa ajili ya kupitia usajili wa
wachezaji wote walioombewa katika dirisha dogo wakiwemo wale wa mkopo. |
No comments:
Post a Comment