Laurence Mafuru
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete amemteua Bwana Laurence Nyasebwa Mafuru kuwa Msajili wa Hazina
kuanzia tarehe 5 Novemba, 2014.
Taarifa
iliyotolewa jana Desemba 11, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi
Ombeni Y. Sefue inasema kuwa kabla ya uteuzi wake, Bwana Mafuru alikuwa
Mkuu wa Idara ya Rasilimali Fedha katika Ofisi ya Rais inayohusika na
ufuatiliaji Miradi ya Matokeo Makubwa Sasa (PDB). Aidha Bwana Mafuru
pia alikuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Benki ya FBME iliyowekwa chini ya
uangalizi wa muda wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Wakati
huohuo, Taarifa ya Balozi Sefue inasema Rais Kikwete amemteua Bibi
Beng’i Mazana Issa kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi kuanzia tarehe 4 Desemba, 2014. Kabla ya uteuzi
wake, Bibi Mazana Issa alikuwa Mkurugenzi wa Utawala wa Fedha katika
Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS).
Rais
pia amemteua Profesa Dominic M. Kambarage kuwa Makamu Mkuu wa Chuo
Kikuu Kipya cha Kilimo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuanzia
tarehe 5 Desemba, 2014.
Taarifa
hiyo ilisema kabla ya kuteuliwa kwake kuwa Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa
Kambarage alikuwa Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Sokoine, Morogoro.
Taarifa
ya Balozi Ombeni Sefue imesema kufuatia kuanzishwa kwa Chuo hicho
kingine cha Umma, Rais Kikwete pia amemteua Profesa Lesakit S. Mellau
kuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho upande wa Taaluma kuanzia tarehe 5
Desemba, 2014, na kabla ya uteuzi wake, Profesa Mellau pia alikuwa
Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Sokoine, Morogoro.
Aidha
Taarifa ya Balozi Sefue imesema Rais Kikwete amemteua Profesa Msafiri
M. Jackson kuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere (Utawala) kuanzia tarehe 5 Desemba, 2014. Kabla ya
uteuzi huo, Profesa Jackson alikuwa Mratibu wa Masomo ya Taaluma za
Shahada za Juu katika Chuo Kikuu cha Ardhi, Dar es Salaam.
|
No comments:
Post a Comment