Wakati leo Mkoa wa Iringa ukiadhimisha wiki ya Usalama Barabarani yenye kauli
mbiu 'Maamuzi yako barabarani ni hatima yetu - fikiri kwanza', Ajali
mbaya iliyohusisha gari dogo lenye namba za usajili T 570 BHK imetokea kwenye msitu wa Mafinga Iringa leo mchana na kusababisha kifo cha mtu mmoja. Kwa mujibu wa habari
zilizotikia aliyepoteza maisha ni Yunith
Gwamaka Mwakenja. Waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni dereva wa gari hilo ambaye ni mhadhiri wa
chuo cha Tumani Makumira tawi la Mbeya Bw. Gwamaka Mwakenja pia
majeruhi mwingine ni Joyce Fredy.
Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika. |
No comments:
Post a Comment